Staa wa Bongo Movie Kajala Masanja aliwahi kuwa mgeni wangu kwenye studio za #TZA na millardayo.com katikati ya mwezi April 2015, nakumbuka jibu lake kuhusu ishu ya Wema kutokua na uwezo wa kuzaa; “Mwandishi
alinipiga mwandishi akaniulizaa kuhusu hiyo kitu.. nikamwambia namwonea
huruma, yeye bado mdogo asikate tamaa kwamba hatozaa.. labda atafute
Doctor mzuri kama kweli ana nia ya kupata mtoto atapata..“
Saa moja muda mfupi uliopita kaandika post yenye ujumbe huu alafu kaweza na picha ya Wema Sepetu na Petit Man>>> “BINADAMU
TULIUMBWA KUISHI KATIKA MISINGI YA UBINADAMU NA SIO UNYAMA KAMA
WAISHIVYO WANYAMA WA PORINI LEO NAOMBA KUSEMA KUTOKA MOYONI MWANGU..
NAJUA KABISA NINA WAZAZI WANGU NDUGU ZANGU NA ZAIDI SANA MUNGU WANGU ILA
KUNA WATU MPAKA NAKUFA KAMWE SINTOWASAHAU KATIKA KUTA ZA MOYO WANGU
KATIKA KIPINDI CHANGU KIGUMU NILICHOPITIA MLIKUWA NEMBO NA MBONI KUBWA
KATIKA KUOKOA MAISHA YANGU… NAPENDA KUSEMA KUWA HATA KWA HAYA YOTE
TUNAYOPITIA BADO NI MADOGO SANA KUFICHA THAMANI YENU MLIYOIJENGA JUU
YANGU..NAKUMBUKA SANA MLIPOJITOA KWA AJILI YANGU MLIPOJINYIMA KWA AJILI
YANGU MLIPOPIGANA KWA AJILI YANGU,MLIVYOFEDHEHEKA KWA AJILI YANGU YOTE
HAYO NAYAKUMBUKA NA NAMSHUKURU MUNGU KWANI NAONA KABISA MLILETWA DUNIANI
KWA SABABU NYINGI NA MOJA YA SABABU ILIKUWA KUNIOKOA KATIKA KIPINDI
KIGUMU KATIKA MAISHA YANGU.LEO HII TAREHE 25.5.2015 NAPENDA KUSEMA KWA
UMMA NA ZAIDI KWA MUNGU WANGU KUWA NAWATHAMINI NAWAPENDA NA NASHUKURUUU
SANA KWA YOTE MLIYOFANYA JUU YANGU.. NAWAOMBEA KWA MUNGU MUENDELEE NA
MOYO HUO HUO KWANI NAAMINI KUNA WENGI BADO WANAWATEGEMEA ILI KUKOMBOA
MAISHA YAO KWA WAKATI ALIYOPANGA MUNGU HATA KITABU CHA DINI
KILISEMA KUWA “huwezi kumpenda Mungu usiyemuona wakati unamchukia ndugu
yako unayemuona” NAJUA SIKU MOJA TUTAISHI KAMA ZAMANI.. AHSANTENI” >>> @new_kajala
Post a Comment