Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe akiwa na Jimmy Mgaya anayedaiwa kuwa ni bwanake.
Achilia mbali akina pedeshee Mangi, Dallas na Gee Modal, kigogo mpya wa staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe safari hii amenaswa laivu wakijiachia kwa raha zao, Risasi Jumamosi lina cha kushika mkononi.
Kwa mujibu wa chanzo, kigogo huyo ni mtu mwenye fedha zake aitwaye Jimmy Mgaya ambaye ni Mbongo mfanyabiashara aishie nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.
Chanzo hicho kilishusha data kuwa jamaa huyo ndiye aliyempangia
Wolper nyumba ya kifahari iliyopo ushuani Mbezi-Beach jijini Dar.Huku
akirusha picha za kimahaba za wawili hao, sosi wetu huyo alisema kuwa
Jimmy ni ‘mtu f’lani hivi amazing’ kwa sababu anakata mkwanja kinoma.
Jacqueline Wolper na Jimmy Mgaya wakipozi kimahaba.
“Kama mtakumbuka kuna siku gazeti lenu (Risasi Jumamosi) mliandika
kuwa Wema (Sepetu) na Wolper walilewa chakari kwenye pati ya ‘bethidei’
ya Petit Man, basi huyo kigogo ndiye aliyewafanyia kufuru na ile pati
ilifanyika nyumbani kwake, Kinondoni-Manyanya (Dar),” kilimwaga ubuyu
chanzo chetu.
Chanzo hicho kilidai kwamba picha za wawili hao wakijiachia ambazo
gazeti hili linazishikilia zilipigwa maskani kwa jamaa huyo huko Durban
kwenye Jimbo la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe.
Baada ya jitihada za kumsaka mwanaume huyo kugonga mwamba, gazeti
hili lilimtwangia simu Wolper na kumsomea mashitaka yake juu ya mwanaume
huyo ambapo mbali na kukiri kumfahamu Jimmy, alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli namfahamu Jimmy, nilikutana naye kwenye mizunguko yangu nje ya nchi. Si kweli kwamba ni bwana’ngu. Kuhusu picha, nilipiga naye kama rafiki tu na sioni kama ni picha mbaya.”
“Ni kweli namfahamu Jimmy, nilikutana naye kwenye mizunguko yangu nje ya nchi. Si kweli kwamba ni bwana’ngu. Kuhusu picha, nilipiga naye kama rafiki tu na sioni kama ni picha mbaya.”
Hivi karibuni Wolper alikiri kuwa na mwanaume lakini akawa anaogopa
kumwanika kwa kuogopa kuporwa na wasichana wa mjini hivyo inaaminika
ndiye huyo Jimmy.
Post a Comment