
Leo asubuhi msanii kutoka Nairobi Kenya
anajulikana kwa jina la COLONEL MUSTAFA alinitumia ujumbe mfupi kupitia
WhatsApp yangu na kuniambia niwajulishe mashabiki wake wote kuhusu
kuhairishwa kwa video yake mpya ya DODOMA SINGIDA.
“Ningependa kujulisha mashabiki wangu kuwa video yA DODOMA SINGIDA ambayo ilifaa kutoka jana tarehe 22/5/2015 itachelewa kidogo kutoka, kutokana na jana mimi kushikwa na police (CID) kwa makosa ambayo nadaiwa kuwa nilitumia model ambaye ni mke wa mtu mashuhuri nchini Kenya bila mumewe kujulishwa kabla ya shooting..kuna madaliko lazima yafanyike ndio video ya dodoma singida iweze kutoka..Asante na nina wapenda wote”

Post a Comment