SHABAAASH! Staa aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia
Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, anadaiwa
kurekodiwa mkanda wa ngono na kusambazwa katika mitandao ya kijamii,
Amani linakupa stori kamili.
Staa aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.
Chanzo cha habari hii kimeeleza kwamba, tukio hilo lilitokea hivi
karibuni baada ya mtu anayedaiwa kuwa ni mchumba wa staa huyo kumrekodi
video hiyo na baadaye walipopishana kauli, akaamua kuisambaza kwa njia
ya CD.
“Jana bwana niliona video ya utupu ya Jini Kabula ikiuzwa kitaani kwetu katika CD jambo ambalo ni aibu sana,” alisema mtoa ubuyu wetu, mkazi wa Manzese, jijini Dar.
“Jana bwana niliona video ya utupu ya Jini Kabula ikiuzwa kitaani kwetu katika CD jambo ambalo ni aibu sana,” alisema mtoa ubuyu wetu, mkazi wa Manzese, jijini Dar.
Amani lilishuhudia baadhi ya picha zinazodaiwa kuwa zilikatwa kutoka
katika video hiyo ndipo mwanahabari wetu alipomvutia waya Jini Kabula
ili kujua nini kilimsibu hadi akarekodiwa video hiyo.Alisema kwa
mazingira ya tukio hilo, anashindwa hata ajibu nini maana haelewi
kilichotokea hadi mkanda huo ukasambaa kiasi hicho na kumsababishia
matatizo kwa ndugu zake.
“Kiukweli nashindwa hata nikujibu nini maana kama aibu tayari
imeshanikuta, hivyo sioni kama naweza kuongea kitu chochote kwa sasa
kikanisafisha, kikubwa namwachia Mungu maana sina tena pa kuuficha uso
wangu kwa hiki kilichotokea, yaani yamenikuta,” alisema Jini Kabula
ambapo alipobanwa zaidi kuhusu aliyemrekodi, alijibu kuwa ni mchezaji wa
timu ya Yanga pasipo kumtaja jina.
“Bwana ni mchezaji wa Yanga, alikuwa mtu wangu.”
“Bwana ni mchezaji wa Yanga, alikuwa mtu wangu.”
Post a Comment