Serikali itaongeza mshahara wa watumishi wa umma kwa asilimia 13 .5 katika mwaka ujao wa fedha wa 2015/16.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Manejimenti ya Utumishi wa Umma),
Celina Kombani, (pichani), alisema bungeni wakati akihitimisha mjadala
wa bajeti ya ofisi hiyo.
Hata hivyo, alisema ongezeko hilo litapandisha mishahara ya kima cha chini zaidi huku cha juu kikiongezwa kwa asilimia 3.0.
Awali wabunge wakichangia bajeti yake walitaka mishahara
ikipandishwa iwanufaishe watumishi wa chini kwa vile inapopanda kwa
asilimia 10 mtumishi wa chini ambaye mshahara wake ni Sh. 265,000
anapata nyongeza ya Sh. 30,000.
Hata hivyo, kwa wenye mishahara inyoanzia Sh. 3,000,000 wanafaidika zaidi kwa nyongeza ya 300,000.
Kombani alisema wenye mishahara minono wanalipa kodi kubwa ya mshahara ya lipa kiasi unavyopata (Paye) kwa asilimia 30.
Kwa kutumia maelezo hayo mtu mwenye mshahara wa Sh. 3,000,000, atalipa Paye ya Sh. 900,000.
Akizungumzia ajira ya walimu alisema taifa limeajiri walimu wa
kutosha na sasa inajielekeza kwenye maeneo mengine ya kilimo na afya.
Alisema mwaka unaoishia wa 2014/15 walimu walikuwa 31,000 wakati sasa wataajiriwa 28,957.
Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye, alitaka sheria irekebishwe ili mawaziri wapewe pensheni.
Post a Comment