Meja jenerali Godefroid Niyombare
Kumekuwa
na mapigano usiku kucha katika mji mkuu wa Burundi ambako kulikuwa na
jaribio la mapinduzi ya kutaka kumng’oa madarakani rais, Pierre
Nkurunziza.
Rais huyo ameshindwa kurejea nchini mwake kutoka
katika mkutano wa viongozi wa kanda,baada ya ndege yake kugeuza kurejea
ilikotokea.
Ingawa askari watiifu kwa rais huyo wamedai kuzima
jaribio hilo la mapinduzi yaliyokuwa yakiongozwa na meja jenerali
Godefroid Niyombare dhidi ya rais wao,na kwamba udhibiti wan chi uko
mikononi mwao na hasa katika maeneo muhimu ya mji mkuu wan chi hiyo
,Bujumbura.
Makabiliano ya risasi yamesikika karibu na vituo vya
redio na runinga .mwandishi wa BBC aliyeko nchini Burundi amesema kwamba
ameshuhudia jeshi likiwa limegawanyika pande mbili ,na haijulikani nani
ameshikilia udhibiti wa nchi kwa sasa.
Rais Nkurunziza
amekosolewa kwa haja yake ya kuwania muhula wa tatu wa uongozi nchini
Burundi ,maamuzi ambayo yalisababisha wiki kadhaa za maandamano ambapo
watu ishirini wameripotiwa kupoteza maisha.

إرسال تعليق