Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Kazi Maalum),
Profesa Mark Mwandosya, anatarajia kutangaza nia ya kugombea urais Juni
Mosi na kuchukua fomu Juni tatu mwaka huu.
Mwandosya ambaye tayari ametangaza kuacha kuwani ubunge katika
jimbo la Rungwe Mashariki, anakusudia kuchukua fomu siku hiyo kuwania
mbio za urais.
Profesa Mwandosya alisema sababu zilizomsukuma kuwania urais, atazitaja Juni Mosi atakapotangaza nia mkoani Mbeya.
Alisema Sababu za kutaka kuwania urais na nini nitawafanyia
watanzania, akiingia madarakani ataeleza siku ya kutangaza nia Juni
Mosi.
Waziri Mwandosya ni mmoja kati ya makada wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) ambao kwa muda mrefu wameonesha nia ya kutaka kumrithi Rais Jakaya
Kikwete anayemaliza muda wake.
Waziri Mwandosya aliwahi kuwania urais mwaka 2005 na kushika nafasi
ya tatu akiwafuatia Dk. Salim Ahmed Salim na Raos Jakaya Kikwete
aliyeibuka mshindi.
Post a Comment