Taswira
za machafuko nchini Burundi wakati wa maandamano ya kupinga hatua ya
Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza ya kuamua kugombea tena katika
uchaguzi mkuu ujao nchini humo.
Polisi wawili wameuawa katika machafuko yanayoendelea nchini Burundi
katika mwendelezo wa maandamano ya wapinzani ya kupinga hatua ya Rais wa
nchi hiyo Pierre Nkurunziza ya kuamua kugombea katika uchaguzi mkuu
ujao nchini humo.
Polisi ya Burundi imetangaza kuwa, mbali na polisi hao wawili, mtu
mmoja mwengine alipoteza maisha katika shambulio hilo lililotokea jana
usiku jijini Bujumbura. Kwa mujibu wa mashuhuda, shambulio hilo
lilitokea majira ya saa moja na nusu usiku katika eneo la Kamenge,
kaskazini mashariki mwa mji huo.
Maandamano ya kupinga uamuzi wa Rais Nkurunziza kutaka kugombea
katika uchaguzi wa rais ujao, yamezorotesha uchumi wa nchi hiyo. Hayo
yanajiri katika hali ambayo rais huyo ameendelea kushikilia msimamo wake
wa kugombea kwenye uchaguzi huo.
Akihutubia sherehe za Mei Mosi hapo jana, Rais huyo kijana, mbali na
kukosoa maandamano ya wapinzani aliwataja watu wanaoandamana kuwa ni
watoto wadogo wanaojiingiza katika mambo yasiyowahusu.
إرسال تعليق