STAA
wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameacha aibu ya aina yake
barani Ulaya baada ya gauni lake kuvuka na kuacha ‘nido’ zake hadharani,
Risasi Mchanganyiko lina stori kamili.
Staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiimba kwa hisia.
Tukio hilo lililozua gumzo katika mitandao mbalimbali ya kijamii,
lilijiri usiku wa kuamkia Jumatatu iliyopita katika Jiji la Antwepen,
Ubeligiji wakati Shilole aliyeambatana na mpenzi wake Nuh Mziwanda
walipokuwa wamekwenda kutumbuiza katika ukumbi unaofahamika kwa jina la
Togenblink.
Kwa mujibu wa chanzo, akiwa jukwaani, Shilole alipandwa na mzuka wa
aina yake wakati akitumbuiza nyimbo zake kali ndipo nguo zake
zilipojiachia na kusababisha nido zake kuonekana, hali iliyowapa mhemko
wa namna yake wanaume waliohudhuria shoo hiyo.
Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, mwanahabari wetu ‘alimvutia waya’
Shilole moja kwa moja nchini humo ili kujua nini kilitokea, mwanamuziki
huyo alifafanua hivi:
“Ishu ilikuwa hivi, mimi nilikuwa kwenye mzuka wa shoo, kuna mtu
ambaye alikuwa ananifuatilia tu kila ninalofanya jukwaani ili aniharibie
kwa sababu hakufurahishwa na mimi kufanya shoo na Manganga One
(muandaaji).
“Alichokifanya yeye ni kuniwinda pale bahati mbaya braa iliposhuka kutokana na mishemishe za kucheza, akapiga picha hiyo kisha akaiweka mitandaoni ili kunikomoa,” alisema Shilole.
“Alichokifanya yeye ni kuniwinda pale bahati mbaya braa iliposhuka kutokana na mishemishe za kucheza, akapiga picha hiyo kisha akaiweka mitandaoni ili kunikomoa,” alisema Shilole.
Alipoulizwa sababu za mtu huyo kumtegea picha hiyo, Shilole alisema
alimkatalia kufanya shoo yake kwa kumueleza kuwa hawezi kufanya shoo
yake kabla hajamalizana na Manganga One ambaye ndiye alikuwa amewahi
kuomba huduma yake.
إرسال تعليق