Na Modewji blog team
SERIKALI na Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jana wametiliana saini mkataba
utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni
nchini.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja
wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira
Rodrigues (wa pili kulia), Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing
(kushoto), Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha (kulia),
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar
pamoja na mkalimani wa Balozi wa China wakifurahi jambo wakati Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome
(hayupo pichani) akiwasili kwenye chumba cha mikutano Wizara ya Elimu
kwa ajili ya hafla fupi ya kutiliana saini mkataba utakaowezesha
kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini.
(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Akizungumza baada ya kutiwa saini kwa
mkataba huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa
Sifuni Mchome alisema mradi huo ni mkombozi mkubwa katika maandalizi ya
kufundisha kwa kutumia Tehama nchini.
Alisema mpango huo wenye kuwezesha walimu
kujifunza Tehama unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China
ambao ndio wamepitisha fedha zao UNESCO.
Katika utiaji saini huo ambapo Balozi wa
China nchini Dk. Lu Youqing alikuwepo, katika jumla ya uhai wa mradi
ambao ni miaka miwili , miundombinu ya ufundishaji masomo ya sayansi na
hesabu katika vyuo vya walimu vya Monduli na Tabora itaboreshwa.
Katika mradi huo walimu watafundishwa elimu ya Tehama, namna ya kufundisha na kujifunza.
Katibu mkuu Mchome alisema kwamba vyuo hivyo
viwili vitawezeshwa kuwa na mtandao ambao utaunganishwa na vyuo vingine
vinane vya masomo ya sayansi na hesabu kwa ajili ya kubadilishana
taaluma.
Pia vyuo hivyo vitawezeshwa kuandaa programu
zenye kuelezea mfumo wa utoaji huduma za Tehama kwa ajili ya walimu wa
masomo ya sayansi na hesabu.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja
wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira
Rodrigues (katikati) akisalimina kwa furaha na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome (kulia) na kushoto ni
Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing (aliyeipa mgongo kamera).
Profesa Mchome alisema ili taifa liweze
kusonga mbele katika mpango wake wa kufundisha kwa kutumia Tehama ni
vyema kuandaa walimu na fedha za China kupitia Unesco zitasaidia
maandalizi hayo.
“Tunaamini tukiwekeza katika vifaa vya
kupromoti Tehama, walimu wakifundishwa na kuandaliwa vyema, wataenda
kusaidia kufundisha na kuwezesha matumizi ya Tehama katika shule zao.”
Alisema Profesa Mchome.
Alisema japo zipo program ndogo nyingine ,
program waliyotia saini jana ilikuwa kubwa na yenye tija
itakayoimarisha ubora wa elimu kwa kuwapa wanafunzi elimu ya
kujitegemea, elimu yenye kuwakwamua kiujuzi na kuutumia ujuzi huo kwa
maendeleo yao na taifa.
Tanzania ni miongoni mwa mataifa barani
Afrika ambayo mapema wametambua thamani ya kufundisha kwa njia ya Tehama
ili kuboresha elimu na mfumo wa elimu.
Taasisi zitakazohusika na mradi huo ni
pamoja na Chuo Kikuu Huria (OUT) na Taasisi ya Elimu nchini(TIE) kwa
kuratibiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni
Mchome (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi.
Zulmira Rodrigues (katikati) pamoja na Balozi wa China nchini, Mh. LU
Youqing (kushoto) kabla ya kutiliana saini mkataba huo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza jambo
kabla ya kusaini mkataba huo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome na Kulia ni Kaimu Katibu
Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi. Waliosimama
wakishuhudia tukio hilo kutoka kushoto ni Joel Nanauka wa UNESCO, Afisa
tawala msaidizi wa UNESCO, Rahma Islem, Afisa mipango wa utamaduni wa
UNESCO, Rehema Sudi, Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing, Ofisa
anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar pamoja
na Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome
wakitiliana saini mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa
kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini unaofadhiliwa na Serikali ya
Jamhuri ya watu wa China. Wanaoshuhudia tukio hilo waliosimama ni Balozi
wa China nchini Tanzania, Mh. LU Youqing (wa pili kushoto), Ofisa
anayeshughulikia masuala ya elimu kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar (wa
pili kulia), Afisa mipango wa utamaduni wa UNESCO, Rehema Sudi
(kushoto), Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha na Kulia
aliyeketi ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi
Kimizi.
Zoezi la kusaini mkataba likiendelea.
Wakifurahi kwa pamoja mara baada ya zoezi la kutia saini kukamilika.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues
(kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa
Sifuni Mchome wakibadilishana hati za mkataba utakaowezesha kutekelezwa
kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini unaofadhiliwa na
Serikali ya Jamhuri ya watu wa China. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Balozi
wa China nchini Tanzania, Mh. LU Youqing(wa pili kushoto) pamoja na
Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha (kulia).
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues
akizungumza jambo baada ya kutiliana saini mkataba huo.
Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha (kulia)
akizungumza jambo na Afisa wa ubalozi wa China (katikati) na Kushoto ni
Afisa Utawala msaidizi wa UNESCO, Rahma Islem.
إرسال تعليق