Hofu ya ugaidi imezidi kutanda katika wilaya ya kilombero baada ya
watu sita kujeruhiwa vibaya na bomu lililorushwa kwa mkono wakati
wakitoka katika maadhimisho ya mei mosi katika kijiji cha msolwa
ujamaa kata ya sanje wilayani kilombero mkoani Morogoro .
Katika hospitali ya ST KIZITO MIKUMI walikolazwa majeruhi wa tukio
hilo wamesema bomu hilo lilirushwa na vijana wawili baada ya
kutiliwa shaka na wananchi wa kijiji cha msolwa ujamaa kata ya sanje
tarafa ya mangula kuwaweka chini ya ulinzi kwa ajili ya kuwapekua ambapo
vijana hao walirusha bomu na kujeruhi wananchi pamoja na baadhi ya
viongozi wa serikali waliokuwa kwenye gari ya mweneyekiti wa halmashauri
wakitokea katika maadhimisho ya mei mosi ambapo wameomba jeshi la
polsi kufanya uchunguz kufuatia matukio yanayoashiria ugaidi kuendelea
kuandama wakazi wa kilombero.
Nao viongozi wa kata akiwemo diwani wa kata ya sanje David Ligazio
wamesema ipo haja ya serikali kuongeza nguvu ya jeshi la polisi ikiwa
ni pamoja na magari ya usafiri na kutafuta vifaa vinavyo weza kuchunguza
maeneo ya milima ya udizungwa na Ruaha ambapo wamebaini wahalifu
wengi wamewaona wakitokea katika misitu hiyo mara kw amara.
Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Lenard Pual amedhibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema hadi sasa jeshi la polisi
linawatafuta watuhumiwa hao ambao baada ya kurusha bomu hilo limejeruhi
dereva wa mweneyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kilombero na
kuharibu gari ya halmshauri pamoja na wananchi wa kijiji cha msolwa
ujamaa.
Tukio hilo limetokea ndani ya siku 14 baada ya watuhumiwa 9
kukamatwa msikitini wakiwa na milipuko 30, sare za jeshi, bendera nyeusi
pamoja na vitu mbalimbali vya kufanyia uhalifu huku mmoja akichomwa
moto na wananchi wenye hasira akiwa katika harakati za kutoroka baada ya
kumchoma askari kwa jambia shingoni katika tarafa ya kidadu wilayani
kilombero.
ITV
إرسال تعليق