MKURUGENZI wa Endless Fame,
Wema Isaac Sepetu, juzikati alionesha maajabu ya aina yake baada ya
kuwagaragaza waigizaji wenzake Jacqueline Wolper, Elizabeht Michael
‘Lulu’, na Riyama Ally katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Watu.
Mkurugenzi wa Endless Fame, Wema Isaac Sepetu akiwa ameshika tuzo yake.
MKURUGENZI wa Endless
Fame, Wema Isaac Sepetu, juzikati alionesha maajabu ya aina yake baada
ya kuwagaragaza waigizaji wenzake Jacqueline Wolper, Elizabeht Michael
‘Lulu’, na Riyama Ally katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Watu.
Wadau mbalimbali waliohuzuria wakufuatilia hafla hiyo ya utoaji tuzo.
Tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Mei, 23 mwaka huu katika Hoteli
ya Hyatt Regency iliyopo Posta jijini Dar es Salaam.Wema aliibuka kinara
na kuwafanya baadhi ya mashabiki wake walipuke kwa shangwe huku Wolper,
Lulu na Riyama wakibaki kimya.
Mkurugenzi wa Endless Fame, Wema Isaac Sepetu akiwa na Meneja wake Martin Kadinda.
Akizungumza kwa furaha muda mfupi baada ya kutwaa tuzo hiyo, Wema
alisema kwamba amefurahia kuwa mshindi na amejisikia vizuri kwani
hakutarajia kuibuka kidedea, ila anaamini mashabiki wake ndiyo
waliomfanya akashinda na kuahidi kuwa nao bega kwa bega.
“Nashukuru sana kwa kutwaa tuzo hii ambayo kwa namna moja au nyingine
naiona kama sapraizi maana tulikuwa tukigombea wengi, ila mashabiki
wangu wameniwezesha kwa kiasi kikubwa kuitwaa tuzo hii, ninachoweza
kusema kwa sasa nashukuru sana uongozi wa Endless Fame hususan meneja na
wafanyakazi wangu wote,” alisema Wema.
إرسال تعليق