YAMETIMIA--HAYA NDIO LOWASA ALIYOWAAMBIA WATANZANIA LEO



BAADA ya Kimya kizito hatimaye Edward lowassa, naweza kusema ameamua kuvunja ukimya huo na kuibuka kutamka wazi wazi kwamba anaitaka Nafasi ya Urais ndani Chama cha Mapinduzi CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa hapo baadae mwaka huu .Anaripoti KAROLI VINSENT endelea nayo.
       Kuibuka kwa Lowassa ambaye ni Waziri mkuu aliyejiuzulu kwa Kashfa ya Ufisadi kwenye Kampuni  Tata ya Richmound ,kuna kuja siku moja kupita baada CCM kutangaza rasmi tarehe kwa makada wake kuanza kuchukua Fomu ya kuwania kwenye uongozi mbali mbali kwenye Uchaguzi mkuu hapo baadae .
       Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli CCM ameisema kauli hiyo leo Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amesema yupo Vizuti katika kuwania nafasi ya Urais na anatarajia kutangaza rasmi hapo Jumamosi ya wiki hii.
   “Nataka kuwahakikishia nyinyi na watanzania niko vizuri kwa teyari kwa chochote na nipo sawa kuwania nafasi ya Urais ambayo natarajia kutangaza hapo Jumamosi”amesema Lowassa.
       Lowassa ambaye pia ni Mwenyikiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano kimataifa amesema kutokana na tatizo la kubwa la Vijana kukosa Ajira ndio miongoni mwa sababu iliomfanya ajitose kwenye Nafasi hiyo kubwa na uongozi wanchi.
“Tatizo la Ajira ni Bomu ambalo linatarajia kuripuka na,kwakuwa  wako vijana wengi wamemaliza Vyuo vikuu hawana Ajira wapo mitaani unategemea nini,wakati wenzetu katika nchi zilizoendelea katika kipindi cha Kampeni wanaweka wazi mambo ya Ajira, na sio kuwekeza kwenye Kilimo Kwanza na hata chama changu wanajua kwamba sera ya Kilimo kwanza siikubaliani nayo unaitaji taifa liloendelea kwa kuwekeza kwenye Elimu.”
   
KUHUSU AFYA YAKE
Lowasa amesema kuhusu suala la Afya ni amedani ni chuki tu  ipo kwenye  Chama chake cha CCM.
“Kuna chuki imeingia ndani ya chama chetu na mimi nasema chama chetu waweke utaratibu wa kupima Afya ambao tunagombania nafasi ya Urais  waweke utaratibu wa kufanya hivyo na mimi nawahakikishia nipo vizuri”amesema Lowassa.
 
   KUHUSU KUHAMA CCM.
Lowassa pia alizungumzia suala hilo ambalo mara kwa mara lilikuwa likiandikwa kwenye magazeti ambayo yalikuwa yakidai endepo atakatwa jina lake ndani ya CCM atajiunga kwenye Chama kipya cha kisiasa cha ACT-Wazaendo.
Ambapo lowassa amesema hawezi kuhama chama hicho kikongwe kilichopo barani Afrika.
          “Kuhama chama sina mpango nimeamia CCM mwaka 1977 sijafanya kazi sehemu popote zaidi ya CCM maisha yangu yote yapo CCM anayetaka nihame basi ahame yeye”.
  
VIJEMBE KWA UTAWALA WA KIKWETE.
Sanjari na kuweka mipango ya kuwaokoa Vijana pia Mwanasiasa huyo Mkongwe akusita kutoa Vijembe kwa Rais anayemaliza mda wake Rais Jakaya kikwete kwa kusema limefika hapo kwenye matatizo kutokana na kuwa kwa watendaji wabovu wanaofanya kazi kimazoea.
     
KUHUSU MADAI ANAYODAI NI YA VISASI.
Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM amesema kuhusu Visasi kwamba yeye ni ni Mkristo na hana Visasi na mtu yeyote.
“Mimi ni Mkristo hata bwana yesu alisema samehe mara sabini sina kisasi na mtu  yeyote”
   
KUHUSU HALI YA UPINZANI.
Mbali na mambo hayo pia Lowassa amezungumzia hali ya vyama vya Upinzani na ameikitaka chama chake kisizubae.

“Nachoweza kusema kwamba Upinzani umepata nguvu,mijini na Vijijini, sisi ni chama kinachoshika Dola tusizubae na wenzetu wameanza pata nguvu tusibweteke,maana wenzetu wamejiandaa vizuri,na sisi tunapaswa kujipanga maana Vyama vya Ukombozi Afrika vimeondolewa kwahiyo tusijisahu maana ukitoka madakani urudi”

Post a Comment

أحدث أقدم