Bodi ya mikopo kuboresha huduma katika kupambana na migomo


kilango
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela.
Na Georgina Misama, MAELEZO-Dodoma
Katika kuboresha mahusiano kati ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu na   Tume ya Vyuo Vikuu na kuondosha migomo na maandamano ya wanafunzi  dhidi ya Bodi, serikali imeweka muwakilishi wa Tume ya Vyuo Vikuu kuwa mjumbe kwenye Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Akijibu swali Bungeni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela amesema pia chuo kimeelekezwa kuajiri Afisa atakayeshughulikia masuala ya mikopo na kuwa kiungo kati ya wanafunzi, Chuo na Bodi ya Mikopo.
Mhe. Malecela alikua akijibu swali lililoulizwa ma Mhe. Suzan Lyimo (Viti maalum) aliyetaka kujua matokeo ya tume maalum iliyoundwa kuchunguza utendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Mhe. Malecela amesema kuwa Tume hiyo ilibaini kuwa pamoja na mambo mengine mawasiliano hafifu kati ya Bodi ya Mikopo, Tume ya vyuo vikuu, Taasisi za Elimu ya juu na Wanafunzi ndio  yanasababisha migomo na maandamano ya wanafunzi wa Elimu wa Juu.
Amesema utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Tume iliyoundwa kuchunguza yamefanikiwa kuondosha migomo na maandamano hayo
Aidha, Bodi ya Mikopo imeboreshwa kwa kuajairi watumishi wenye sifa stahiki na vitendea kazi vya kutosha. Aidha, Bodi ya Mikopo imeanzisha ofisi katika kanda za Dododma, Zanzibar na Mwanza ili kuwahudumia wadau wa karibu.

Post a Comment

Previous Post Next Post