
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela.
Na Georgina Misama, MAELEZO-Dodoma
Katika
kuboresha mahusiano kati ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu na Tume ya
Vyuo Vikuu na kuondosha migomo na maandamano ya wanafunzi dhidi ya
Bodi, serikali imeweka muwakilishi wa Tume ya Vyuo Vikuu kuwa mjumbe
kwenye Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Akijibu
swali Bungeni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne
Kilango Malecela amesema pia chuo kimeelekezwa kuajiri Afisa
atakayeshughulikia masuala ya mikopo na kuwa kiungo kati ya wanafunzi,
Chuo na Bodi ya Mikopo.
Mhe.
Malecela alikua akijibu swali lililoulizwa ma Mhe. Suzan Lyimo (Viti
maalum) aliyetaka kujua matokeo ya tume maalum iliyoundwa kuchunguza
utendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Mhe.
Malecela amesema kuwa Tume hiyo ilibaini kuwa pamoja na mambo mengine
mawasiliano hafifu kati ya Bodi ya Mikopo, Tume ya vyuo vikuu, Taasisi
za Elimu ya juu na Wanafunzi ndio yanasababisha migomo na maandamano ya
wanafunzi wa Elimu wa Juu.
Amesema utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Tume iliyoundwa kuchunguza yamefanikiwa kuondosha migomo na maandamano hayo
Aidha,
Bodi ya Mikopo imeboreshwa kwa kuajairi watumishi wenye sifa stahiki na
vitendea kazi vya kutosha. Aidha, Bodi ya Mikopo imeanzisha ofisi
katika kanda za Dododma, Zanzibar na Mwanza ili kuwahudumia wadau wa
karibu.
إرسال تعليق