Eugene Mwaiposa enzi za uhai wake.
MBUNGE wa Jimbo la Ukonga, Eugene Mwaiposa (CCM) amefariki dunia
akiwa nyumbani kwake mkoani Dodoma leo baada ya kusumbuliwa na shinikizo
la damu kwa muda mrefu.
Taarifa imetolewa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ni kwamba alikuwa na tatizo la shinikizo la damu kwa muda mrefu
na amefariki akiwa nyumbani kwake Dodoma.
Ameongeza kuwa nyumbani kwa marehemu ni eneo la Chaduru jirani na jengo jipya la Hoteli ya Shabiby barabara ya Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu umepelekwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi.
Mwili wa marehemu umepelekwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi.
Shughuli ya kuaga mwili itafanyika kesho. Naibu Spika ametumia kanuni
ya 152 kuahirisha bunge hadi keshokutwa Alhamisi kutokana na msiba huo.

إرسال تعليق