HII ni dunia ya mambo mengi! Mkazi wa Kigogo -Luhanga jijini Dar,
aliyefahamika kwa jina la baba Juma, Jumamosi iliyopita alijikuta
akitimuliwa ukweni sanjari na mkewe, Mwanahamisi Njama kwa madai amekuwa
akishindwa kutoa ushirikiano wakati wa kuchangia chakula kwenye familia
ya mkewe.
Baba Juma akitimuliwa ukweni.
Katika sakata hilo, baba Juma inasemekana amekuwa akiishi ukweni hapo
ambapo masuala ya msosi wanachangia kwa zamu na familia nzima kila
mmoja na siku yake.Kwa mujibu wa chanzo chetu, zamu ya wanafamilia
wengine ikifika hununua chakula chenye mvuto kinywani, kama samaki wa
Mwanza (sangara, sato) na mapochopocho mengine lakini zamu ya
Mwanahamisi, mumewe hutoa pesa ya matembele jambo linalodaiwa lilikuwa
likiwakera wanafamilia hao.
Kufuatia kero hiyo, kwa mujibu wa chanzo, wanafamilia hao inadaiwa
waliamua kumvalia njuga baba Juma na kumtimua yeye na mkewe na mtoto wao
Juma mwenye miaka miwili.
Ni wakati mtafaruku huo wa ‘aondoke huyo’ ukiwa umepamba moto, chanzo
chetu hicho kilipiga simu Ofisi za Global Publishers, Kitengo cha
Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ na kupasha mchezo kamili na akusema kuwa
timbwili hilo lilikuwa likiendelea ‘laivu’….Bila kuchelewa, mmoja wa
makachero wa OFM kwa kutumia pikipiki iendayo kasi, ndani ya dakika
chache alifika eneo la tukio na kukuta baadhi ya wanafamilia hao
wakiendelea kuwafanyia timbwili Mwanahamisi na mumewe ikiwemo kuwapa
vichapo huku wasamaria wema wachache wakijaribu kutuliza.
Bila
kuchelewa, paparazi wetu alianza kuwafotoa picha wanafamilia hao huku
Mwanahamisi akijaribu kuokoa maisha yake kwa kukimbia huku amembeba
mwanaye.Mwanahamisi alisikika akisema hawezi kuhama nyumbani hapo kwa
vile nyumba hiyo ni ya baba yake mzazi hivyo ni bora wamtenge kwenye
misosi lakini si kumfukuza kabisa.
Utetezi wake ulipingwa vikali na wanafamilia hao hasa mama yao mdogo aliyefahamika kwa jina la mama Hashimu.
Baada ya varangati kuzidi, Mwanahamisi aliona ni heri ambebe mwanaye na kukimbia naye huku mumewe akimfuata kwa nyuma na kwenda kusikojulikana.
Baada ya varangati kuzidi, Mwanahamisi aliona ni heri ambebe mwanaye na kukimbia naye huku mumewe akimfuata kwa nyuma na kwenda kusikojulikana.
Mke wa baba Juma nae akitimuliwa pamoja na mwanaye.
Katika hali ya kushangaza, wanafamilia hao walimgeukia paparazi wetu
na kutaka kumfanyia vurugu ikiwemo kujaribu kuvunja kamera yake lakini
wakagonga mwamba.Katika sakata hilo, mwanadada mmoja aliyekuwa amesahau
kuchana nywele, akiwa amejifunga kanga moja kifuani, nyingine kiunoni
huku hana viatu, alimporomoshea matusi paparazi wetu ambayo aliyarekodi.
Kwa vile kisa kilisikika wakati wa mzozo, gazeti hili lilifanya
jitihada za kuzungumza na wanafamilia hao ili kusikia kutoka kwao lakini
ilishindikana baada ya kukosa ushirikiano kutokana na hasira za kupigwa
picha.
إرسال تعليق