UBABE? WASANII katika tasnia ya filamu, Irene Paul ‘Smart
Girl’ na Halima Yahaya ‘Davina’ wamejikuta wakitaka kuzichapa kavukavu
baada ya kushindwa kudhibiti hasira walipokuwa wakitaniana.
Mwandishi wetu aliyeshuhudia tukio hilo mita chache na mahali alipokuwa, alishuhudia Davina naye akimpa maneno makali mwenzake ndipo wakataka kuzichapa lakini bahati nzuri wakaamuliwa.

Irene Paul
Ishu hiyo ilitokea juzikati ndani ya Viwanja vya Leaders Club,
Kinondoni jijini Dar, kulipokuwa na mkusanyiko wa wasanii mbalimbali
ndipo wawili hao walipotunishiana misuli.
Halima Yahaya ‘Davina’
Ishu hiyo iliibuka baada ya Davina kumtupia maneno ya kejeli mwenzake
huku Irene akionekana kuwa ‘siriaz’ akitahadharisha kuwa hapendi utani
na kuanza kumtupia maneno makali jambo lililowafanya baadhi ya wasanii
kutuliza hali ya hewa.Mwandishi wetu aliyeshuhudia tukio hilo mita chache na mahali alipokuwa, alishuhudia Davina naye akimpa maneno makali mwenzake ndipo wakataka kuzichapa lakini bahati nzuri wakaamuliwa.
إرسال تعليق