
MKAZI
wa Mpiji Magoe Hamis Mohameid (21), amefikishwa kizimbani jana katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Dar es Salaam akikabiliwa na tuhuma
za kumbaka mwanafunzi (14)Jina limehifadhiwa na kumpa mimba.
Akisomewa
mashtaka mawili mbele ya Hakimu Flora Mtarania, Wakili wa Serikali
Grace Lwila, alidai kuwa tukio hilo lilitokea kati ya Aprili na Mei24
mwaka huu maeneo ya huko Mpiji Magoe.
Katika
shtaka la kwanza Wakili alidai kwamba mtuhumiwa alimbaka msichana huyo
kisha kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.
Wakili
Lwila alidai kuwa katika shtaka la pili katika tarehe isiyojulikana
maeneo ya Mpiji Magoe mtuhumiwa alimpa ujauzito mwanafunzi huyo wa
kidato cha pili anayesoma shule ya Sekondari Mpiji Magoe.
Mtuhumiwa
alikana kutenda shtaka hilo na upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea
ambapo Hakimu Mtarania alisema kwamba shauri hilo linadhaminika.
“Unatakiwa
ulete wadhamini wawili walioajiriwa kutoka serikalini au katika taasisi
inayotambulika kisheria watakaoweka bondi ya maandishi ya Sh. Milioni
1,” alisema Mtarania.
إرسال تعليق