KIWANGO! Tofauti na watu wengine ambao maumbile yao
hubadilika mara baada ya kujifungua, kwa staa wa sinema za Kibongo, Aunt
Ezekiel hali imekuwa tofauti, uzuri na umbo lake limebaki vilevile.
“Nachukia ubonge nyanya, namshukuru Mungu pia kwani wengi wakijifungua huwa wananenepa hovyo lakini kwangu mambo yamekuwa tofauti. Niko vilevile, nafikiri pia ni kutokana na kufuata ushauri mzuri wa kula chakula niliopewa,” alisema Aunt.
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel akiwa na mwanaye.
Akizungumza
nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar, Aunt alisema kilichomfanya
asinenepe kupita kiasi na kuharibika mwili ni mazoezi sambamba na
kufuata ushauri wa vyakula anaopewa hivyo mwili wake kubaki vilevile.“Nachukia ubonge nyanya, namshukuru Mungu pia kwani wengi wakijifungua huwa wananenepa hovyo lakini kwangu mambo yamekuwa tofauti. Niko vilevile, nafikiri pia ni kutokana na kufuata ushauri mzuri wa kula chakula niliopewa,” alisema Aunt.
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel.
Mbali na kutobadilika, Aunt alisema kwa sasa muda mwingi anautumia
kuwa nyumbani na ubavu wake, Moze Iyobo wakimlea mtoto wao tofauti na
zamani alipokuwa na misele ya usiku katika viwanja tofauti vya starehe.
Post a Comment