MASKINI MTOTO HUYU

Mtoto (2)Inatia huruma, sehemu ya haja kubwa ya Mtoto Yathib Rajab.
Boniphace Ngumije na Chande Abdallah
MASKINI mtoto huyu! Unapojaliwa kupata mtoto akiwa mzima asilimia 100 unatakiwa kumshukuru Mungu. Mwajuma Juma (25) mkazi wa Mbagala, Sabasaba Dar es Salaam, ameingia kwenye mtihani mzito tangu ajifungue mwanaye Yathib Rajab mwaka mmoja uliopita, akiwa hana sehemu ya kujisaidia haja kubwa.
Mtoto (3)Mwajuma Juma akiwa na mwanaye Yathib Rajab.
Baada ya kugundulika kuwa na tatizo hilo madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili walimfanyia opasuaji na kumtoboa kwenye tumbo lake upande wa kulia na kuchomoa sehemu ya utumbo ambayo imekuwa ikitumika kumsaidia mtoto huyo kujisaidia.
Mtoto (1)Mwajuma Juma akimbembeleza mwanaye Yathib Rajab..
Akizungumza na Ijumaa juzi, Mwajuma alisema kuwa madaktari walimwambia kuwa Aprili mwaka huu alitakiwa kurudi hospitalini hapo ili wamfanyie upasuaji wa kumtengenezea sehemu ya kutolea haja kubwa.
“Madaktari waliniambia utaratibu wa kuwasaidia bure watoto wenye tatizo hili umesogezwa mbele mpaka mwaka 2019. Ili sasa afanyiwe upasuaji zinahitajika shilingi 1,350,000 ambazo sina kwani baba wa mtoto huyo alifariki dunia wakati nina mimba ya miezi sita.
Naomba msaada kwa Watanzania wenzangu ili mwanangu afanyiwe upasuaji, anateseka sana,” alisema mama huyo.
Yeyote aliyeguswa na tatizo la mtoto huyu anaweza kutuma chochote au kuwasiliana na mama yake kwa namba 0652 082 464.

No comments:

Post a Comment