
Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (OWM) – TAMISEMI (Elimu), Mhe.
Kassim Majaliwa (MB) (aliyevaa miwani) akisalimiana na viongozi pamoja
na wazazi wa wanafunzi wa shule ya msingi Munguli, kata ya
Mwangeza,tarafa ya Kiru mi, wilayani Mkalama wakati wa ziara ya siku
moja wilayani humo kutembelea maeneo ya wanayoishi wanafunzi wa jaamii
ya kabila la Wahaadzabe.

Wanafunzi
wa shule ya msingi Munguli wakiimba wimbo wa shule yao wakati
wakimpokea Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (OWM) – TAMISEMI
(Elimu), Mhe. Kassim Majaliwa (MB) alipowatembelea shuleni kwao.

Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (OWM) – TAMISEMI (Elimu), Mhe.
Kassim Majaliwa (MB) akiongeaa na wazazi pamoja na walezi wa wanafunzi
wa shule ya msingi Munguli.

Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (OWM) – TAMISEMI (Elimu), Mhe.
Kassim Majaliwa (MB) (wa kwanza kutoka kushoto) akisikiliza maoni,
ushauri pamoja na maswali kutoka kwa wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo.

Baadhi
ya wazazi wa wanafunzi wa jamii ya kabila la wahadzabe wakimsikiliwa
Mh. Majaliwa alipokuwa akaiongea nao kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo.

Baadhi
ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama pamoja na baadhi ya
wanafunzi wa shule ya msingi Munguli (waliovaa sare za shule).

Baadhi
ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama pamoja na wazazi wa
wanafunzi wa shule ya Msingi Munguli wakimsikiliza Mh. Kassimu Majaliwa
(hayupo pichani).
Na Jumbe Ismailly,Mkalama
NAIBU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (OWM) – TAMISEMI (Elimu), Mhe.
Kassim Majaliwa (MB) amemwagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya
wilaya ya Mkalama kuhakikisha anawajengea matundu ya vyoo wanafunzi wa
jamii ya kabila la wahadzabe wa kike wa shule ya msingi Munguli ili nao
waweze kupata sehemu ya kujisaidia kwa nafasi badala ya ilivyo sasa
ambapo wanachangia na wavulana.
Naibu
waziri huyo, Kassimu Majaliwa alitoa agizo hilo alipokuwa akiongea na
wazazi na wanafunzi wa shule ya msingi Munguli,iliyopo katika Kata ya
Mwangeza,tarafa ya Kirumi kufuatia taarifa ya mkurugenzi huyo kwamba
wanafunzi wa kike na wale wa kiume wanachangia matundu ya vyoo.
“Na
leo nimemwambia mkurugenzi kati ya bweni na bweni kuna choo pale cha
matundu mawili,ananiambia huku wavulana na kule
wasichana,haiwezekani,tuamue tu lile jengo liwe la wavulana peke yao au
wasichana peke yao’alibainisha naibu waziri huyo.
Alisema
Majaliwa kwamba ni vyema wasichana wakajengewa matundu ya vyoo eneo
mbali na wavulana ili kuwaepusha kukutana na wavulana hususani nyakati
za usiku,kwani endapo utaratibu ulipo sasa utaendelea utahatarisha
maisha ya wanafunzi hao wa kike watakapokuwa wakikutana usiku na
wavulana chooni.
Hata
hivyo Majaliwa hakusita kujizuia furaha yake kutokana na kitendo
kilichofanywa na mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone cha kuifufua
shule hiyo iliyojengwa katika kipindi cha utawala wa baba wa
taifa,marehemu Julius Kambarage Nyerere,iliyokuwa imeanza kupoteza
umaarufu wake.
Naye
afisa elimu wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama,Mwisungi Kigosi
alielezea changamoto zinazoikabili shule ya msingi Munguli kuwa ni
pamoja na upungufu wa matundu ya vyoo vya
wanafunzi,madawati,meza,viti,kabati,uhaba wa maji,chakula,mafuta ya
kupikia,chumvi,sabuni na nguo za kubadilisha wanafunzi wa bweni.
Hata
hivyo licha ya kuwepo kwa changamoto hizo,afisa huyo mwenye dhamana ya
kusimamia sekta ya elimu alibainisha utatuzi wa changamoto hizo kuwa ni
Miss Tanzania namba tatu ambaye pia ni Miss Singida namba moja Miss
kanda ya kati, Dorice Mollel ametoa msaada wa mablanketi 40 pamoja na
vitabu.
Aidha
Kigosi alisema pamoja na Miss Singida huyo kutoa msaada huo,vile vile
aliahidi kutafuta wadau wa maendeleo kujenga maktaba ya kisasa
itakayotumika kwa ajili ya wanafunzi hao.
Kwa
upande wao baadhi ya wazazi na walezi wa wanafunzi hao,mwenyekiti wa
jamii ya kabila la wahadzabe,Edward Mashimba alielezea kero
zinazowakabili wananchi wa eneo hilo kuwa ni pamoja na ubovu wa
barabara,mawasiliano ya simu na uvamizi katika hifadhi ya msitu
waliokuwa wakiutegemea kujipatia chakula.
Wilaya
ya Mkalama ina jumla ya vituo vitatu vya elimu nje ya mfumo rasmi
(MEMKWA) katika shule za msingi Mwanga,Nkungi na Chemchemu huku ikiwa na
shule binafsi moja inayomilikiwa na shirika la Dini la Roman Catholic
yenye jumla ya wanafunzi 189,ambao kati yao wavulana ni 84 na wasichana
ni 105.
Post a Comment