
Katibu
wa CCM wilaya ya Ikungi,Aluu Segamba, akizungumza kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika katika kijiji cha Puma kwa ajili ya Katibu Mkuu
UVCCM Taifa, Sixtus Raphael Mapunda kuzungumza na wananchi.

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Taifa, Sixtus Raphael Mapunda akitema cheche katika mkutano huo wa hadhara.

Mkazi
wa kijiji cha Puma tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida,
Seleman Nkhomee, aliuliza swali kuwa ni lini CCM itaanza kuwalipa posho
mabalozi wa nyumba kumi. Mzee Nkhomee aliuliza swali hilo kwenye mkutano
wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya Katibu Mkuu UVCCM Taifa,Sixtus
Raphael Mapunda(hayupo pichani).

Mkazi
wa kijiji cha Puma tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi, mzee Karani
Kidamui aliuliza swali juu ya matumizi ya gunia aina ya Lumbesa ambayo
alidai yanatumika kudhulumu wakulima wa viazi vitamu.Mzee Karani
aliuliza swali hilo kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya
Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Sixtus Raphael Mapunda.

Mkazi
wa kijiji cha Puma tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi mkoani Singida
Christina Andrew, akiuliza swali kuwa alama nyekundu iliyopo kwenye
bendera ya CHADEMA, inamaanisha nini.Hata hivyo mama huyo hakuweza
kupatiwa jibu baada ya kukosekana kwa mwanaCHADEMA ndani ya mkutano
huo.

Mbunge
wa kuteuliwa na rais Dkt.Grace Khwaya Puja,akitoa nasaha zake kwenye
mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya Katibu Mkuu UVCCM Taifa,
Sixtus Raphael Mapunda.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Ikungi -Singida
KATIBU
Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Taifa, Sixtus Raphael
Mapunda, amewahimiza wazazi/walezi nchini, kuongeza juhudi zaidi kuwalea
watoto wao katika maadili mema, ili kudhibiti kasi kubwa ya mmomonyoko
wa maadili ambayo ina madhara mengi ikiwemo tishio la uhai wa wazazi na
walezi.
Mapunda
ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara
uliohudhuriwa na wanaCCM na wananchi wa kata ya Puma jimbo la Singida
magharibi wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Akifafanua,
alisema uzoefu unaonyesha wazi kwamba mmomonyoko wa maadili
umewafikisha vijana wengi katika hatua mbaya ya kudharau na kutokuwatii
wazazi/walezi na jamii inayowazunguka.
“Nimepewa
taarifa kwamba baadhi ya vijana katika wilaya ya Ikungi, wakati wa
chaguzi mbalimbali, wamekuwa wakiwanyang’anya kwa nguvu kadi za kupingia
kura wazazi/walezi wao kwa lengo likiwa ni kumnyima haki mzazi kuchagua
chama na kiongozi anayempenda”, alisema Mapunda.
Alisema
vitendo vya aina hiyo vinakwenda kinyume na Katiba ya Jamhuri
inayomtaka kila mtu kuwa huru kuchagua kiongozi anayemtaka au chama
anachoamini kitamsaidia kujiletea maendeleo.
“Vijana
kama wamefikia hatua hiyo ya kumnyang’anya haki mzazi au mlezi, basi
ipo siku itafika anaweza hata kumkatisha maisha ya hapa duniani”,
alisema kwa masikitiko.
Katika
hatua nyingine, Mapunda ambaye pia ni MNEC, amewataka wananchi wa
wilaya ya Ikungi waisome kwa kina Katiba iliyopendekezwa,ili waweze
kujijengea mazingira mazuri wakati wa kuipigia kura.
“Katiba
hii mpya iliyopendekezwa ni nzuri mno kwa sababu imezingatia maslahi ya
makundi yote ya Watanzania. Mimi huwa nawashangaa sana viongozi wanao
hamasisha wananchi waipigie kura ya hapana katiba hii ambayo imekidhi
mahitaji yote ya Watanzania kwa zaidi ya miaka 50 ijayo”alisema Katibu
huyo.
Akifafanua
zaidi ,Mapunda alisema katiba mpya iliyopendekezwa ina kifungu
kinachosema kwamba kila mtu ana uhuru wa kuishi sehemu yo yote katika
nchi yake ya Tanzania.
“Wapo
viongozi na hapa kwenu wapo, ambao wanatumia nguvu nyingi kuhamasisha
wananchi kukataa katiba iliyopenekezwa kwa maana kwamba wanataka wakatae
kuishi nchini mwao kwa uhuru mpana, utakawasaidia kuwapa fursa ya
kujiletea maendeleo”,alisema Katibu huyo.
Mapunda
alisema viongozi na hasa wa kutoka upande wa upinzani,wamejenga
utamaduni mbaya wa kukataa kila kitu hata kiwe na maslahi kwa
wananchi.Amedai kitu cho chote kibaya,kinatoka CCM.
“Hofu
yangu ni kwamba mpinzani akijenga akilini mwake kwamba vitu vyote au
matukio yote mabaya yanachangiwa na CCM, basi ipo siku mwanaume wa
upande wa upinzani atakaposhindwa kumpatia mimba mke wake, ataisingizia
CCM ndiyo imesababisha matokeo hayo” ,alisema Mapunda na kushangiliwa
kwa nguvu na wananchi.
Post a Comment