Mmomonyoko wa maadili kufikisha vijana katika hatua mbaya ya kudharau


DSC06344
Katibu wa CCM wilaya ya Ikungi,Aluu Segamba, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Puma kwa ajili ya Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Sixtus Raphael Mapunda kuzungumza na wananchi.
DSC06388
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Taifa, Sixtus Raphael Mapunda akitema cheche katika mkutano huo wa hadhara.
DSC06412
Mkazi wa kijiji cha Puma tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Seleman Nkhomee, aliuliza swali kuwa ni lini CCM itaanza kuwalipa posho mabalozi wa nyumba kumi. Mzee Nkhomee aliuliza swali hilo kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya Katibu Mkuu UVCCM Taifa,Sixtus Raphael Mapunda(hayupo pichani).
DSC06416
Mkazi wa kijiji cha Puma tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi, mzee Karani Kidamui aliuliza swali juu ya matumizi ya gunia aina ya Lumbesa ambayo alidai yanatumika kudhulumu wakulima wa viazi vitamu.Mzee Karani aliuliza swali hilo kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Sixtus Raphael Mapunda.
DSC06417
Mkazi wa kijiji cha Puma tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi mkoani Singida  Christina Andrew, akiuliza swali kuwa alama nyekundu iliyopo kwenye bendera ya CHADEMA, inamaanisha nini.Hata hivyo mama huyo hakuweza kupatiwa jibu baada ya kukosekana kwa mwanaCHADEMA ndani ya mkutano huo. 
DSC06355
Mbunge wa kuteuliwa na rais Dkt.Grace Khwaya Puja,akitoa nasaha zake kwenye mkutano wa hadhara  ulioitishwa kwa ajili ya Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Sixtus Raphael Mapunda.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Ikungi -Singida
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Taifa, Sixtus Raphael Mapunda, amewahimiza wazazi/walezi nchini, kuongeza juhudi zaidi kuwalea watoto wao katika maadili mema, ili kudhibiti kasi kubwa ya mmomonyoko wa maadili ambayo ina madhara mengi ikiwemo tishio la uhai wa wazazi na walezi.
Mapunda ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wanaCCM na wananchi wa kata ya Puma jimbo la Singida magharibi wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Akifafanua, alisema uzoefu unaonyesha wazi kwamba mmomonyoko wa maadili umewafikisha vijana wengi katika hatua mbaya ya kudharau na kutokuwatii wazazi/walezi na jamii inayowazunguka.
“Nimepewa taarifa kwamba baadhi ya vijana katika wilaya ya Ikungi, wakati wa chaguzi mbalimbali, wamekuwa wakiwanyang’anya kwa nguvu kadi za kupingia kura wazazi/walezi wao kwa lengo likiwa ni kumnyima haki mzazi kuchagua chama na kiongozi anayempenda”, alisema Mapunda.
Alisema vitendo vya aina hiyo vinakwenda kinyume na Katiba ya Jamhuri inayomtaka kila mtu kuwa huru kuchagua kiongozi anayemtaka au chama anachoamini kitamsaidia kujiletea maendeleo.
“Vijana kama wamefikia hatua hiyo ya kumnyang’anya haki mzazi au mlezi, basi ipo siku itafika anaweza hata kumkatisha maisha ya hapa duniani”, alisema kwa masikitiko.
Katika hatua nyingine, Mapunda ambaye pia ni MNEC, amewataka wananchi wa wilaya ya Ikungi waisome kwa kina Katiba iliyopendekezwa,ili waweze kujijengea mazingira mazuri wakati wa kuipigia kura.
“Katiba hii mpya iliyopendekezwa ni nzuri mno kwa sababu imezingatia maslahi ya makundi yote ya Watanzania. Mimi huwa nawashangaa sana viongozi wanao hamasisha wananchi waipigie kura ya hapana katiba hii ambayo imekidhi mahitaji yote ya Watanzania kwa zaidi ya miaka 50 ijayo”alisema Katibu huyo.
Akifafanua zaidi ,Mapunda alisema katiba mpya iliyopendekezwa ina kifungu kinachosema kwamba kila mtu ana uhuru wa kuishi  sehemu yo yote katika nchi yake ya Tanzania.
“Wapo viongozi na hapa kwenu wapo, ambao wanatumia nguvu nyingi kuhamasisha wananchi kukataa katiba iliyopenekezwa kwa maana kwamba wanataka wakatae kuishi nchini mwao kwa uhuru mpana, utakawasaidia kuwapa fursa ya kujiletea maendeleo”,alisema Katibu huyo.
Mapunda alisema viongozi na hasa wa kutoka upande wa upinzani,wamejenga utamaduni mbaya wa kukataa kila kitu hata kiwe na maslahi kwa wananchi.Amedai kitu cho chote kibaya,kinatoka CCM.
“Hofu yangu ni kwamba mpinzani akijenga akilini mwake kwamba vitu vyote au matukio yote mabaya yanachangiwa na CCM, basi ipo siku mwanaume wa upande wa upinzani atakaposhindwa kumpatia mimba mke wake, ataisingizia CCM ndiyo imesababisha matokeo hayo” ,alisema Mapunda na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi.

Post a Comment

أحدث أقدم