Mrembo aliyejitambulisha kwa jina la Ester Eliakim, mkazi wa Kinyerezi,
Dar ameibuka na kueleza kwamba alizaa na staa wa filamu Bongo, Kulwa
Kikumba ‘Dude’ ambaye baadaye alimtelekeza yeye na mwanaye Cleopatra
(mwenye miezi 11).
Staa wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Akizungumza na paparazi wetu, Ester alisema mara ya kwanza alikutana
na Dude katika mchezo wa Bongo Dar es Salaam alikokuwa akicheza kama
askari na wakaanzisha uhusiano wa kimapenzi tangu mwaka 2008.
Waliendelea na uhusiano wao wa siri huku Dude akimtaka awe msiri ili kuilinda familia yake jambo ambalo alikubali.
Mwaka jana alipata ujauzito na kumweleza Dude ambaye alikubaliana naye na akawa anamhudumia, lakini kwa sharti la kumtafuta kijana na kumfanya mpenzi kivuli ili awe ndiye aliyempa mimba, kwani ikijulikana ni wake itakuwa ni shida kwa mkewe Eva.

“Baada ya mtoto kuzaliwa niliyembambika alipomuona tu alikataa nilipomueleza Dude akakataa kunihudumia, kodi ilipoisha alinitumia hela nusu.
“Kila ninapowasiliana naye, ananipiga chenga niko tayari kupima DNA
kwa sababu nina uhakika 100% mtoto ni wa Dude,” alisema Ester.Gazeti
hili lilimtafuta supastaa Dude, lakini hakupokea simu wala kujibu sms
alizotumiwa zaidi ya kuandika “Niko kwa Benard Membe, nipigie baadaye.”
Post a Comment