MUIGIZAJI
mahiri wa filamu, Slim Mbegu ‘Slim’ hivi karibuni aliangua kilio akiwa
Mahakama ya Mwanzo Magomeni baada ya kushuhudia gari alilopewa zawadi
yeye na mkewe aliyetengana naye, Asia Morgana likivutwa kwa Break Down
kusogezwa eneo hilo.
Muigizaji mahiri wa filamu, Slim Mbegu ‘Slim’.
Wawili hao walikuwa na shauri mahakamani hapo wakigombea gari hilo
kila mmoja akidai ni mali yake halali, lakini hatimaye mwanamke
alishindwa na hivyo Slim kuamriwa kulipeleka kortini ili liweze
kukabidhiwa kwa wenyewe, lakini akashindwa kwa kushindwa kulifanyia
matengenezo madogomadogo ya kulifanya litembee.
Gazeti hili liliongea na Asia aliyemshukuru Mungu kwa kuweza kupata
gari lake alilodai kusumbuliwa kwa muda mrefu na aliyekuwa mumewe,
wakati Slim alisema hana la kusema zaidi ya kumuachia Mungu kila kitu.
Post a Comment