
Kabla sijaianza mada ya leo inayosomeka “Si lazima mumeo akuanze
mnapokuwa faragha” niwape pole ndugu zangu ambao mko kwenye mfungo wa
Ramadhani, leo ni siku ya kumi na tatu mkiwa kwenye swaum Mungu awatie
wepesi mmalize salama.
Nikiuliza mjitokeze mashoga ambao mna uwezo wa kuwaanza waume zenu
muwapo faragha ni hakika yangu kuwa wengi wenu mtainamisha vichwa chini
au kuangalia pembeni mkimaanisha ni vigumu sana kuonesha uhitaji kwa
waume wenu.
Lakini niwaambie tu mashoga zangu hakuna kitu kizuri kinachoweza
kumfurahisha mumeo kama kuonesha kuwa unahamu ya kukutana naye pale
muwapo kwenye uwanja wenu wa kujidai.
Bila shaka anapofanya hivyo kwako unajisikia furaha eeh, unatambua ni
kwa namna gani unahamasa hadi mumeo anakuwa na hamu ya kukutana nawe,
sasa kama ilivyo kwako ndivyo inavyoweza kuwa kwa mumeo pia.
Jenga utaratibu hata bila kumwambia kuwa mtakuwa na zamu, kakuanza
leo, wakati mwingine mkutanapo usisubiri tena hadi ‘kigogo wako’
akunyemelee ukiwa umejikausha ‘kau’, onesha kumhitaji zaidi, mfuate hadi
mahali alipo anza utundu wako uliojaliwa utamtia hamasa aelewe kuwa
kazi anayoifanya si haba.
Shoga hata siku moja hutakiwi kuwa baridi chumbani, ikiwa unampango
wa kudumisha ndoa moja ya sehemu muhimu kudumisha ni mahali hapo,
ukiharibu mimi simo ‘habari ya mjini’ nimekupa.
Mwanamke shupavu hata siku moja si muoga, anajua anachokifanya
usisubiri yakukute uanze kwenda kwa waganga, jenga ndoa kwa busara zako
mwenyewe.
Leo nimemaliza tukutane Jumanne nyingine panapo majaliwa.
Leo nimemaliza tukutane Jumanne nyingine panapo majaliwa.
إرسال تعليق