Mwisho wa jeuri? Mzazi mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Emmanuel
Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson anadaiwa kumwangukia
mwanamuziki huyo ili warudiane walee mtoto wao.

Kwa upande wake mama Nay alisema yeye ndiye alikuwa mtetezi wake lakini kwa sasa hataki kusikia ishu hiyo.
Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’
Habari kutoka chanzo cha kuaminika ambacho ni ndugu wa Siwema
kilieleza kuwa, pamoja na maneno ya shombo aliyommwagia Nay wakati
wanaachana, mrembo huyo kwa sasa ameweka silaha chini akiomba wawe kama
zamani.
Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa katika pozi na Siwema Edson.
Kilidai kwamba hivi karibuni, mmoja wa dada wa Siwema (jina
linahifadhiwa) amekuwa akimpigia simu Nay akimuomba arudishe moyo wake
kwa Siwema, kwani tangu aachane naye mambo yamekuwa yakienda kombo
ikiwemo ule msala wa kesi inayoendelea mahakamani ya kujipatia mali
isivyo kihalali.

Ney wa mitego , Siwema Edson wakiwa na mtoto wao.
Baada ya kumwagiwa ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilituma kijumbe
kumfikishia Nay ombi hilo la Siwema ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Kweli nimepokea simu za msamaha. Nimemsamehe lakini siwezi kurudiana
naye.”Kwa upande wake mama Nay alisema yeye ndiye alikuwa mtetezi wake lakini kwa sasa hataki kusikia ishu hiyo.
إرسال تعليق