NI shiida! Siku chache baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya
nchini, Esterlina Sanga ‘Linah’ kulalamika juu ya kitendo cha Wema
Sepetu ‘Madame’ kumchukua aliyekuwa bwana’ake Nangari Kombo, muigizaji
huyo ameibuka na kutoa maneno yanayoashiria kejeli, kuwa aache presha,
kwani zile ni picha tu!
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madame'.
Katika gazeti la Risasi Jumamosi, toleo lililopita, iliripotiwa na
kuchapishwa habari na picha zilizomuonyesha Madame akiwa amepozi
kitandani na kijana huyo, aliyepata umaarufu baada ya kuingia ndani ya
eneo la kuchezea katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam mwaka
2010, wakati wa mechi kati ya Brazil na Taifa Stars na kumkumbatia
kiungo nyota wa mabingwa hao wa zamani wa dunia, Kaka.
Lakini Risasi Mchanganyiko lilipotaka kujua maoni yake juu ya shutuma
hizo, Wema alisema kupiga picha na Nangari hakumaanishi mapenzi, kwani
yeye ni mtu wa watu na picha kama hizo hupiga na marafiki zake wengi tu,
hivyo Linah asiwe na shaka naye hata kidogo.
“Nilipiga naye kama ninavyoweza kupiga na marafiki wengine kama akina
Martin Kadinda, Petit Man na wengineo. Sina uhusiano naye wa kimapenzi,
naomba aamini kuwa ni rafiki tu wa kawaida,” alisema Wema na kuibua
maswali juu ya aina ya uswahiba wa kawaida wa kupiga picha kitandani na
mpenzi wa mtu!
إرسال تعليق