CRISTIANO RONALDO NAHODHA MTARAJIWA REAL MADRID

CRISTIANO RONALDO huenda akaukwaa unahodha wa Real Madrid iwapo Sergio Ramos atafanikiwa kujiunga na Manchester United.
Ramos bado yuko 'vitani' na mabosi wa Real Madrid akiwataka wamruhusu atimkie zake Old Trafford.
Kocha mpya wa Real Madrid Rafa Benitez anatarajiwa atamchagua Ronaldo kuwa nahodha wake kutokana ukweli kuwa baada ya Ramos ni yeye tu na Marcelo ndio wachezaji waliodumu Madrid kwa muda mrefu.
Marcelo beki wa Brazil alijiunga na Real Madrid mwaka 2007 wakati Ronaldo aliingia mwaka 2009 akitokea Manchester United.
Hata hivyo Marcelo hana uhakika wa kuwa na namba ya kudumu, hali inayotoa mwanya kwa Ronaldo kutwaa unahodha kirahisi.

Post a Comment

Previous Post Next Post