Mchekeshaji
maarufu Eric Omondi na bendi ya muziki ya SARABI kutoka Kenya
wataungana na wanamuziki wa Tanzania Grace Matata na Leo Mkanyia na
bendi yake ya Swahilli Blues kukonga nyonyo za mashabiki wa muziki na
vichekesho jijini Dar es Salaam wakati wa onyesho la muziki jumamosi
wiki hii.
Na Mwandishi Wetu
Mchekeshaji
maarufu Eric Omondi na bendi ya muziki ya SARABI kutoka Kenya
wataungana na wanamuziki wa Tanzania Grace Matata na Leo Mkanyia na
bendi yake ya Swahilli Blues kukonga nyonyo za mashabiki wa muziki na
vichekesho jijini Dar es Salaam wakati wa onyesho la muziki jumamosi
wiki hii.
Onyesho
hilo ambalo limeandaliwa na CDEA:“Culture and Development East Africa”
kwa kushirikiana na Nafasi Art Space litafanyika jumamosi ya tarehe moja
mwezi wa nane mwaka huu, kuanzia saa moja jioni mpaka asubuhi katika
ukumbi wa Nafasi Art Space-Mikocheni.
Mratibu
wa onyesho hilo Naamala Samson alisema kuwa mbali na onyesho hilo pia
kutakuwa na burudani kemkem kutoka kwa maDJ wa Santuri Safari kutoka
Kenya na Uganda ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi 10,000/- kupata
burudani za muziki wa bendi na kwa wale watakaoingia kwenye disco la
kukesha ni shilingi 20,000/-, na tiketi za V.I.P zitauzwa kwa shilingi
40,000/-.
“Wanamuziki
wote wamefanya mazoezi ya kutosha na wamejiandaa kikamilifu kwa onyesho
hili la kihistoria, ni siku hiyo watanzania watapata fursa ya kuonja
ladha ya muziki wa Afrika Mashariki wenye vionjo vya nyumbani na kupata
vichekesho vya mwaka kutoka kwa Omondi” alisema Naamala.
Bendi
ya Sarabi ni miongoni mwa bendi kubwa na zinazofanya vizuri nchini
Kenya na kuwepo kwake kwenye tamasha hili kutanogesha mambo na kutoa
burudani ya kutosha kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani.
Tamasha
hilo limedhaminiwa na Regency Park Hotel, Vibe Magazine, Bongo5.com,
Michuzi Blog, Goethe Institut, Midundo Online Radio, CEFA, Timeticket,
Nafasi Art Space, Eco Sanaa Arts Space, Creative Infinity, Kenya
Airways, Apex Media, Iris Media, Kumkichwa Entertainment, Santuri Safari
DJs na Legendary Music
Post a Comment