Hatimaye
staa wa Bongo Fleva ambaye ni zao la Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT),
Esterlina Sanga ‘Linah’ amechumbiwa rasmi na yule jamaa wake, Wiliam
Bugene ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka kiukoo wa mpenzi wa mwanamuziki
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady.’
Akizungumza
kwenye mahojiano maalum alipotimba katika Tamasha la Filamu la
Kimataifa (ZIFF), Zanzibar hivi karibuni, Linah alisema kuwa ana furaha
maishani mwake kwa kumpata mtu mwenye mapenzi ya kweli ambaye atafunga
naye ndoa ‘soon’.
“Tayari
ameshanichumbia, anajulikana kwetu na mimi najulikana kwao. Kifuatacho
ni ndoa yangu,” alisema Linah ambaye hivi karibuni amesema ataachia
wimbo mpya utakaokuwa gumzo.
Furaha
ya Linah inakuja kufuatia kumpata mwanaume huyo ambaye amekuwa
akionekana naye kila kiwanja wakiwa wamegandana kimahaba ikiwa ni miezi
kadhaa tangu alipodai kuporwa bwana’ke, Nagari Kombo anayedaiwa
kakwapuliwa na Wema Sepetu.
Kabla
ya Boss Mtoto na Kombo, huko nyuma Linah aliwahi kuripotiwa kuwa kwenye
uchumba ‘serious’ na msanii mwenzake, Amini Mwinyimkuu.
Post a Comment