MUNGU mkubwa! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia siha ya mama
mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura
Kassim ‘Sandra’ ambaye kwa sasa yupo fiti baada ya kuugua kwa muda
mrefu.
Mwaka
jana, mama Diamond aliripotiwa kushambuliwa na maradhi yaliyoashiria
kupooza hadi kufikia hatua ya kwenda kutibiwa India kisha kurudishwa
nchini akiwa bado hajapona vizuri.
Chanzo
kilicho karibu na familia ya staa huyo kilieleza kuwa, ugonjwa huo
ambao ulimfanya ashindwe kutembea vizuri, ulimsumbua kwa kipindi kirefu
lakini kwa sasa wanamshukuru Mungu, mama huyo anaweza kutembea mwenyewe
na kuendelea na shughuli zake za kila siku.
“Wee
ile ilikuwa hatari, ameumwa sana jamani mama Diamond. Hadi hatua hii
ambayo amefikia kwa sasa, kwa kweli tunapaswa kumshukuru sana Mungu,
ameteseka vya kutosha, sasa hivi ukimuona, shavu dodo,” kilisema chanzo
hicho.
Mwanahabari
wetu baada ya kupenyezewa habari hiyo, hivi karibuni alitumiwa picha ya
mama Diamond akiwa fiti akitembea barabarani akifanya shughuli zake za
kila siku.
Jitihada
za kumpata mama Diamond azungumzie uzima wake hazikuzaa matunda
kufuatia simu yake ya mkononi kutokuwa hewani lakini Diamond alipatikana
na kusema yeye pamoja na bebi wake, mama kijacho, Zarinah Hassan ‘Zari
The Boss Lady’ wanamshukuru Mungu kwani sasa mama yao yuko vizuri
kiafya.
“Mama
ndiyo faraja yangu siku zote. Kwa kumuona hivi mzima sasa hivi, mimi na
bebi wangu (Zari) tuna amani na tunamshukuru sana Mungu, mama anatembea
na kufanya shughuli zake kama zamani,” alisema Diamond.
CHANZO: GPL
Post a Comment