Mamlaka
ya usafirishaji nchini Ufaransa imesema inachunguza mabaki ya ndege ya
yanayodaiwa kupatikana ndani ya Bahari ya Hindi yanachunguzwa ili
kubaini kama ni ya ndege ya Malaysia ya MH370 iliyopotea bila kuwa na
taarifa zozote kwa muda mrefusasa.
Taarifa kutoka Marekani
zinasema wachunguzihao ambao wameona picha za mabaki hayo wana uhakika
mkubwa kwamba ni ya ndege hiyo ya Malaysia ambapo mabaki hayo ni sehemu
ya bawa la ndege.
Hata hivyo, Wataalamu wa Ufaransa wanasema ni
mapema mno kutoa uhakika kwamba mabaki hayo ni lazima yatakuwa ya ndege
ya Malaysia aina ya Boeing 777 ambayo kupotea kwake kumeleta gumzo la
kidunia.
Watu wapatao 239 waliokuwa wakisafiri na ndege hiyo walipoteza maisha.
Akizungumza
mjini New York Marekani, Waziri wa Usafirishaji wa Malaysia Liow Tiong
Lai amesema nchi yake imetuma wataalamu zaidi kuchunguza mabaki hayo.
"Tunahitaji
kuthibitisha" amekaririwa akisema Waziri Lai,na kusisitiza kuwa kwa
vyovyote vile, mabaki yaliyopatikana yanahitaji kuhakikishwa kabla ya
kuthibitisha zaidi kama ndio hasa mabaki ya MH370
إرسال تعليق