Shani Ramadhani
Liwalo na
liwe! Kinara wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ameahidi
kuambatana na waziri mkuu wa zamani ambaye ni Mbunge wa Monduli kwa
leseni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Edward Ngoyai Lowassa kwenye safari
yake ya kuhamia kwenye muungano wa vyama vya upinzani vinavyounda Umoja
wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Wolper alisema kwa mapenzi aliyonayo kwa Lowassa yupo tayari kwenda kokote hata kama siyo Ukawa.
“Mimi ni ‘Team Lowassa’, atakapohamia
nami niko nyuma yake hata kama siyo Ukawa, nitamfuata, mimi na Lowassa
ni damdam, hilo halina ubishi,” alisema Wolper.
إرسال تعليق