Jerry Muro kaingia kwenye siasa uchawi wa mshitua picha na maelezo vipo hapa


IMG-20150730-WA0014
Kumekuwa na wimbi kubwa la watu maarufu kuingia katika siasa na kutangaza kugombea nyazifa mbalimbali katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadae mwezi Oktoba 2015. Jerry Muro ni mmoja kati ya watu maarufu waliojitokeza kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM.
IMG-20150730-WA0012
Kama ilivyo kawaida kwa chama chochote cha siasa wagombea huwa wanajinadi mbele ya wanachama wa chama husika na kuomba kura, Jerry alipata mkasa ambao mwenyewe anakiri kumtisha. Jerry ambae anaomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa ubunge kwa jimbo la kawe kwa tiketi ya CCM anapata upinzani kwa watiania 20.
IMG-20150730-WA0011
July 30 Jerry Muro akiwa  katika kata ya Msasani Bonde la Mpunga wakati anajinadi walitokea vijana wawili, mmoja akavunja nazi na mwingine akavunja mayai vitu ambavyo vinaashiria imani za kishirikina, Jerry amekiri hali hiyo kumtisha maana mambo hayo amekuwa akiyasikia na sio kuyashuhudia.
“Nimepata athari kwa kiasi kikubwa kwa mfano leo tumekwenda katika kampeni nilipoanza kujieleza nimemwaga sera wakatoka watu wawili mmoja akapasua nazi mwingine akapasua mayai”>>> Jerry Muro
Jerry Muro ameingia katika headlines ya kuwa mmoja kati ya watu maarufu waliotangaza kugombea Ubunge Jimbo la Kawe ambalo mbunge wake wa sasa ni Halima Mdee kutokea CHADEMA

Post a Comment

Previous Post Next Post