Kumekuwa na wimbi kubwa la watu maarufu
kuingia katika siasa na kutangaza kugombea nyazifa mbalimbali katika
uchaguzi mkuu utakaofanyika baadae mwezi Oktoba 2015. Jerry Muro ni mmoja kati ya watu maarufu waliojitokeza kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM.
Kama ilivyo kawaida kwa chama chochote cha siasa wagombea huwa wanajinadi mbele ya wanachama wa chama husika na kuomba kura, Jerry alipata mkasa ambao mwenyewe anakiri kumtisha. Jerry ambae anaomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa ubunge kwa jimbo la kawe kwa tiketi ya CCM anapata upinzani kwa watiania 20.
July 30 Jerry Muro akiwa katika kata ya Msasani Bonde la Mpunga
wakati anajinadi walitokea vijana wawili, mmoja akavunja nazi na
mwingine akavunja mayai vitu ambavyo vinaashiria imani za kishirikina, Jerry amekiri hali hiyo kumtisha maana mambo hayo amekuwa akiyasikia na sio kuyashuhudia.
“Nimepata
athari kwa kiasi kikubwa kwa mfano leo tumekwenda katika kampeni
nilipoanza kujieleza nimemwaga sera wakatoka watu wawili mmoja akapasua
nazi mwingine akapasua mayai”>>> Jerry Muro
Jerry Muro ameingia katika headlines ya kuwa mmoja kati ya watu maarufu waliotangaza kugombea Ubunge Jimbo la Kawe ambalo mbunge wake wa sasa ni Halima Mdee kutokea CHADEMA
إرسال تعليق