JOCKTAN WA MAKEKE AFRIKA AELEZA SABABU ZA KUTUMIA WIMBO WA DIAMOND NA SARIF KEITA KWENYE SLUM FASHION AFRIKA - KENYA

Jina hili linalotikisa Afrika mashariki kwa sasa katika tathnia ya mitindo haswa mitindo ya kiafrika kutoka Tanzania JOCKTAN WA MAKEKE AFRIKA juzi aliwaacha hoi mashabiki wa mitindo nchini Kenya kwa kuonyesha uwezo mkubwa jukwaani licha ya kuwa kulikuwa na wanamitindo wengine wengi kutoka nchi mbali mbali za Afrika,  lakini kikubwa ni vile kwanini aliamua kutumia nyimbo hizo tofauti na wengine?
JOCKTAN WA MAKEKE alijibu hivi " Anha mimi nafanya mitindo ya migumu yaani mitindo ya mu - afrika halisi sasa ni ngumu sana modelz wanapoingia jukwaani kuingia na nyimbo za kimagharibi ambazo ndio zilitawala jukwaa basi nikaenda kwa Dj moja kwa moja ili aweze kunitafutia wimbo wa sarif keita- afrika na hii ndio ilionifanya nionekane bora kwani mahadhi ya wimbo na kilichoonekana jukwaani vilienda sambamba kitu kilichonipa raha sana, na pia ilipofika tym yangu kuwakilisha jukwaani niliingia na wimbo wa Daimond kwan nilikuwa ugenini na Diamond ni international artist na anakubalika kitendo hicho pia kiliwafurahisha mashabiki"



Post a Comment

أحدث أقدم