\Leo
siku nzima nilikuwa nina kikao cha mashauriano na Viongozi wa chama wa
kata zote za mkoa wa Dar es Salaam ( mikutano mikuu ya majimbo 10 ya
Dar) . Jumla ya wajumbe 1023 walihudhuria.
Tumesisitiza
kuwa hatutajiunga UKAWA. Ikumbukwe kuwa tuliomba utaratibu wa kujiunga
UKAWA mwezi Aprili mwaka 2015 na hatujajibiwa rasmi lakini moja ya Chama
ndani ya UKAWA kilitangaza kuwa hawatutaki. Hata juzi kwenye gazeti la
Mawio waliandika kuwa tumefukuzwa UKAWA. Sisi tumeamua kuingia kwenye
uchaguzi wenyewe. Tarehe 10 Agosti 2015 tutatangaza mgombea Urais
tutakayemwunga mkono baada ya mkutano mkuu wa kidemokrasia wa ACT
Wazalendo.
Post a Comment