
KWELI wa mbili havai moja. Nyota ya msanii wa muziki wa kizazi
kipya nchini, Diamond Platnumz, inazidi kung’aa baada ya juzi Jumamosi
kushinda tuzo nyingine ya kimataifa, ikiwa ni wiki moja tu tangu anyakue
tuzo ya MTV MAMA 2015.
Staa huyo wa ‘Mdogo Mdogo’ na ‘Number One’
alinyakua tuzo hiyo katika tuzo za Africans Achievers Awards 2015
zilizofanyika Afrika Kusini.
Ushindi huo umezidi kumfanya Diamond kuzidi
kutusua na kuwafunga mdomo wale wote wanaombeza na wasiomkubali kwa
mafanikio aliyonayo katika anga la kimataifa.
Diamond aliandika kwenye akaunti yake ya Instagram
kuonyesha furaha yake na kumshukuru Mungu kwa ushindi huo ambao umezidi
kumweka matawi ya juu.
“Thanks God gof Keep Blessing my Hustle....African
Artiste of the Year#AfricansAchievers Awards 2015.” Ujumbe huo
ulisomeka hivyo na kuendeelea;
“Shukrani nyingi ziwafikie uongozi wangu kwa
kuhakikisha unanisimamia ipasavyo. Mama Yangu kipenzi Sandrag. My
Beautiful Baby@Zarithebosslady. Media zote na mashabiki zangu pendwa kwa
kuendelea kunisapot bega kwa bega,” alimalizia Diamond katika ujumbe
wake huo.
Wakati akisherehekea mafanikio tayari mkali huyo
tayari yupo kwenye kinyang’anyiro kingine cha kuwania tuzo za AFRIMMA
2015 zinazotarajiwa kutolewa hivi karibuni huko Nigeria
Post a Comment