
MSANII maarufu wa tasnia ya filamu nchini, Wema Sepetu, amekubali matokeo kwenye siasa na kusisitiza kwamba ijapokuwa hakuteuliwa katika mchakato wa ubunge, lakini ataendeleza mapambano ya kusaka maendeleo ndani ya Singida.
Wema ametangaza hivyo muda mfupi baada ya
kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa waombaji wa ubunge viti maalumu
CCM Mkoa wa Singida uliofanyika kwenye ukumbi mkubwa wa kanisa la mjini
hapa.
Wema ambaye alishiriki kwa mara ya kwanza katika
kinyang’anyiro hicho alipata kura 90 na kushika nafasi ya nne kati ya
waombaji 13, wakati Mbunge wa viti Maalumu kwa vipindi vitatu mfululizo ,
Diana Mkumbo Chilolo, aliangushwa baada ya kuwa mshindi wa tatu kwa
kupata kura 182. Mshindi wa kwanza alikuwa ni Aysharose Matenbe
aliyepata kura 311.
“Nitumie nafasi hii kuwashukuru wale walionipa
kura 90 na wale wote walioninyima kura kwa jumla wao, wamenipa hamasa na
ari kubwa kuanza rasmi safari yangu ya kisiasa, Ninachoomba ni Mungu
aendelee kunipa uzima, ili siku moja ndoto yangu hii, iweze kutimia,”
alisema Wema aliyewahi pia kuwa Miss Tanzania mwaka 2006.
Awali mapema Wema alipofika Ofisi ya CCM Mkoa,
alikuwa kivutio kikubwa na kila mwana CCM alipiga naye picha jam bo
lililovuta hisia kuwa anakuba.lika kwa wengi. Baadhi ya wajumbe walidai
kama kujinadi ingekuwa sifa pekee ya kushinda, basi Wema angeshinda
nafasi hiyo
Post a Comment