Wema: Nimekatwa

 
MSANII maarufu wa tasnia ya filamu nchini, Wema Sepetu, amekubali matokeo kwenye siasa na kusisitiza kwamba ijapokuwa hakuteuliwa katika mchakato wa ubunge, lakini ataendeleza mapambano ya kusaka maendeleo ndani ya Singida.
Wema ametangaza hivyo muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa waombaji wa ubunge viti maalumu CCM Mkoa wa Singida uliofanyika kwenye ukumbi mkubwa wa kanisa la mjini hapa.
Wema ambaye alishiriki kwa mara ya kwanza katika kinyang’anyiro hicho alipata kura 90 na kushika nafasi ya nne kati ya waombaji 13, wakati Mbunge wa viti Maalumu kwa vipindi vitatu mfululizo , Diana Mkumbo Chilolo, aliangushwa baada ya kuwa mshindi wa tatu kwa kupata kura 182. Mshindi wa kwanza alikuwa ni Aysharose Matenbe aliyepata kura 311.
“Nitumie nafasi hii kuwashukuru wale walionipa kura 90 na wale wote walioninyima kura kwa jumla wao, wamenipa hamasa na ari kubwa kuanza rasmi safari yangu ya kisiasa, Ninachoomba ni Mungu aendelee kunipa uzima, ili siku moja ndoto yangu hii, iweze kutimia,” alisema Wema aliyewahi pia kuwa Miss Tanzania mwaka 2006.
Awali mapema Wema alipofika Ofisi ya CCM Mkoa, alikuwa kivutio kikubwa na kila mwana CCM alipiga naye picha jam bo lililovuta hisia kuwa anakuba.lika kwa wengi. Baadhi ya wajumbe walidai kama kujinadi ingekuwa sifa pekee ya kushinda, basi Wema angeshinda nafasi hiyo

Post a Comment

أحدث أقدم