TAMASHA la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) 2015
limefungwa rasmi juzi Jumamosi katika Ngome Kongwe, Zanzibar na
kushuhudiwa aliyekuwa nyota wa filamu nchini, Adam Kuambiana ambaye ni
marehemu kwa sasa na mwanadada Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ wakifunika mbaya.
Kwa jumla tamasha la mwaka huu lilifana vilivyo
kwa burudani iliyotolewa na wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya nchi
walioshirikishwa na washindi mbalimbali walitwaa tuzo zilizotolewa kwa
msimu wa mwaka 2014-2015.
Kwa upande wa Tanzania, baadhi ya filamu zake
zilifanya vyema kwa kunyakua tuzo kadhaa huku wasanii wake nao wakifanya
yao, ikiwamo kushuhudia marehemu Kuambiana akiibuka kuwa Mwigizaji Bora
wa Kiume wa Ziff 2015.
Kuambiana aliyefariki Mei mwaka jana na Kidoti kila moja alinyakua tuzo ya Mwigizaji Bora kwa msimu wa mwaka 2014/2015.
Kadhalika filamu mbili za Kibongo zilitusua
kimtindo katika tamasha hilo kwa kunyakua tuzo zikipenya kwenye rundo la
filamu karibu 500 zilizoshiriki kinyang’anyiro hicho kwa mwaka huu.
Filamu hizo ni ‘Mr Kadamanja’ iliyoongozwa na
kuigizwa na marehemu Kuambiana ambayo ndiyo pia iliyompa tuzo
aliyonyakua na nyingine ni Daddy’s Wedding iliyonyakua tuzo mbili.
Tuzo ya kwanza kwa filamu hiyo ile ya Chaguo la
Watu (People’s Choice Award), pia kutoa Mwigizaji bora ambaye ni
marehemu Kuambiana, wakati Daddy’s Wedding ilinyakua tuzo ya ‘Best
Cinematography’ na ile ya Director Bora ambayo ilikwenda kwa Honeymoon
Mohamed.
Mrembo Jokate Mwegelo yeye alinyakua tuzo ya
Mwigizaji Bora wa Kike kupitia filamu ya ‘Mikono Salama’ iliyoandaliwa
na Jacob Steven JB.
Jokate aliandika kwenye mtandao wake kushukuru kwa
ushindi huo na kuelezea ni moja ya mafanikio aliyokuwa akiyaota na
kuwashukuru wote waliompa sapoti katika sanaa yake.
Nayo filamu ya ‘Samaki Mchangani’ ilishinda tuzo
za Best Film in Sound, huku tuzo ya Zuku Best Feature Film ikishinda
filamu ya ‘Kutakapokucha’.
Katika upande wa European African Film Festival Awards, tuzo ya Best African Film ilikwenda kwa WAZI? FM – Dir: Faras Cavallo.
Filamu bora za ukanda wa Afrika Mashariki EAC-EAFN
zilizotwaa tuzo usiku wa kuamkia jana ni pamoja na ‘Going Bongo’ ambayo
imetayarishwa na Dean Matthew Ronalds iliyokuwa filamu bora ya mwaka
kutoka Afrika Mashariki
Post a Comment