
Chanzo kilicho karibu na wawili hao kilipenyeza habari kuwa, Shilole na Nuh Mziwanda walilazimika kupatana baada ya kukutanishwa kwenye bethidei ya Kajala bila kujijua na kuombwa wapatane.
Baada ya kunyaka ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu kwa kutumia vyanzo mbalimbali alifanikiwa kuzipata picha za Shilole na Nuh wakiwa wamekumbatiana kwenye sherehe hiyo iliyofanyika nyumbani kwake, Afrikasana jijini Dar.
Mwanahabari wetu alimvutia waya Kajala ili aweze kuzungumzia tukio hilo ambapo alisema aliamua kuwapatanisha kwa sababu anapenda ‘kapo’ yao hivyo kitendo cha wawili hao kutokuwa pamoja kilikuwa kikimuumiza moyo.
Hata hivyo, baada ya kupatanishwa, wadau wa burudani Bongo ambao hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini, waliwaonya wawili hao kutulia na iwe mwisho kugombana maana si mara ya kwanza kugombana.
Kabla ya kupatanishwa, wawili hao walikuwa wakitupiana madongo mitandaoni wakionesha kuwa hawana dalili za kurudiana lakini hatimaye wamekubaliana kuwa pamoja kwa mara nyingine
إرسال تعليق