Wadau Eneo la Changanyikeni Kwa Karibu Mwezi Mzima Sasa limegubikwa na Ujambazi.
Wezi hao huvamia majumbani Mapema Sana kuanzia saa 2 za usiku watu
wakiwa bado hawajalala. Kinachosikitisha wanavamia na silaha za moto na
hakuna cha maana wanachoiba zaidi ya laptop,Simu na visenti vya Mboga.
Tena mbaya zaidi eneo hili liko Karibu na Jeshi.
Ulinzi shirikishi na Sungusungu yetu mpo Wapi ?
Polisi wa Chuo Kikuu mpo Wapi?
Kamanda Kova tusaidie.
Post a Comment