Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akimkadhi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) cheti
na tuzo katika kipengele cha Uelimishaji bora kupitia Uandishi wa
machapisho na mpangilio bora wa maonyesho, baada ya Umoja wa Mataifa
kuibuka mshindi wa kwanza katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya
biashara ya Sabasaba yalipozinduliwa rasmi. Wanaoshuhudia tukio hilo
ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan
Trade), Jacqueline Mneney Maleko (kushoto) pamoja na Waziri wa Viwanda
na Biashara, Mhe.Dkt. Abdallah Kigoda (kulia).
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaohudumia banda hilo kwenye maonyesho
ya Sabasaba wakisheherekea mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.
UN
Tanzania inawakaribisha Watanzania wote wanaotembela maonyesho sabasaba
kufika katika banda lao lililopo Karume Hall na kuweza kushiriki kutoka
maoni ya juu ya utendaji wa kazi za Umoja wa Mataifa Tanzania kwa njia
ya mtandao wa simu yako bila kutozwa malipo yoyote ukitumia huduma hiyo,
kwa wateja wote mitandao ya Airtel, Tigo na Vodacom.
Jinsi ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), kwa kuandika neno UN au UMOJA WA MATAIFA ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa Vodacom ni namba 15055.
Njia nyingine ya kuwasilisha maoni yako moja kwa moja kupitia mtandao (Online) bofya link hii http://gpl.cc/UN2
إرسال تعليق