Gazeti la MWANANCHI limeandika HAPA kwamba Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amefafanua ishu yake ya
kuchukuliwa na askari wa Takukuru kwa mahojiano muda mfupi baada ya
kuchukua fedha benki huko Lindi.
Nape anayewania ubunge wa Jimbo la
Mtama, jana mchana aliamriwa na maofisa wa Takukuru kufika ofisi zao
baada ya kutoka kuchukua fedha benki ya NMB eneo la Misonobarini mkoa
Lindi.
“Ninadhani hawa jamaa
walipotoshwa. Mimi nimekwenda zangu benki kuchukua fedha, lengo langu ni
kuwalipa mawakala,” alisema Nape jana jioni alipopigiwa simu na
Mwananchi kutoa ufafanuzi na akaongeza kwamba “Wakaja hawa jamaa,
wakajitambulisha kuwa wanatoka Takukuru, wakaniuliza ‘mbona ninachukua
fedha nyingi kipindi hiki?’ Nikawaambia ‘nakwenda kulipa mawakala, na
fedha zenyewe ni hizi Sh3.6 milioni’
‘Basi, tukatoka taratibu tukaenda
ofisini kwao, ni karibu tu na benki. Wakanihoji hata haikumalizika nusu
saa, niliwaambia nataka kulipa mawakala wangu, tena fedha zenyewe
hazitoshi, wako zaidi ya 100′ – Nape Nnauye
Nape aliongeza kusema kuwa walimkamata
na akawaambia kuwa yeye ni mwadilifu >>> “Halafu ninyi, mnaacha
marushwa makubwa makubwa huko, watu wanahonga halafu mnamvizia Nape
masikini kwa Sh3mil?,” alisema.
Nape alielezea kufadhaishwa na tukio
hilo akidai kuwa limetengenezwa kwa ajili ya kumchafua hasa kwa kuwa leo
kuna kura za maoni lakini akasema anaamini yeye ni msafi ambapo Kamanda
wa Takukuru wa Mkoa wa Lindi, Stephen Chami alikiri kumhoji Nape lakini
akasema walijiridhisha kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kulipa mawakala.
“Unajua tuna watu wetu, kwenye maeneo
mbalimbali hasa kipindi hiki cha uchaguzi, tumeweka watu wetu maeneo
mengi, tunataka kukomesha rushwa,”
Post a Comment