Bi. Sophia Mkazi na
Mwenyeji wa Kijiji cha Kasanga Wilayani Kisalawe Mkoani Pwani
akiwakaribisha wageni ambao ni Washiriki wa Shindano la mama shujaa wa
Chakula kijijini huko katika sherehe ya iliyofanyika Kijiji cha
Makumbusho Jijini Dar es salaam Jana. ambapo Programu mzima itaoneshwa
katika Runinga ya ITV kila Siku kuanzia Tarehe 2.08.2015-21.08.2015
kuanzia saa 12 Jioni.
Bw. Godia Kaimu Mwenyekiti
wa Kijiji cha Kasanga akiwakaribisha washiriki wa Shindano la Mama
shujaa wa Chakula Shindano Linaloendeshwa na Oxfam Tanzania kupitia
Kampeni ya Grow Kijijini kwake.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Wilaya ya Kisalawe Bw. Ellioth Phillemon akiwakaribisha washiriki wa
shindano la Mama Shujaa wa Chakula Wilayani Kisarawe.
Kikundi cha Burudani na
sanaa cha Rumumba Theatre wakiendelea na Burudani wakati wa sherehe
hizo za ukaribisho kijiji cha Makumbusho.
Eluka Kibona, Meneja
Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea kwa ufupi juu ya Mchakato mzima
wa Shindano la Mama shujaa wa chakula ambalo linalenga kuwawezesha
wakina mama kutambulika katika kilimo na kueleza Matakwa yao juu ya
kilimo endelevu.
Bi. Mwanaidi Hamza ambaye
anatoka katika Programu ya Big Result now akitoa ushuhuda jinsi gani
alivyofanikiwa kulingana na Proramu hiyo na sasa anamaisha mazuri, na
kuwasihi wakina mama wasikate tamaa katika kilimo.
Mkurugenzi Msaidizi Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Jackson Samwel akiwapongeza
Shirika la Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow kuanzisha shindano la Mama
shujaa wa Chakula , kwa kutambua umuhimu wa ardhi katika kuzalisha
chakula, ameshauri akinamama wabadilishane uzoefu pindi watakapokuwa
kambini ili kuja na mbinu mpya za kilimo, ufugaji na uvuvi.
Mmoja wa watoa Burudani, Mwanamke huyu akionesha kuhusu swala zima la Kilimo Endelevu.
Stephen Mfuko aka Zero
akitaja namba za washiriki na Jinsi ambavyo wanaweza Pigiwa Kura ambapo
Programu mzima itaoneshwa katika Runinga ya ITV kila Siku kuanzia
Tarehe 2.08.2015-21.08.2015 kuanzia saa 12 Jioni.
Wageni waalikwa katika sherehe hiyo.
Ofisa wa Programu ya
Kampeni ya Grow Tanzania Suhaila Thawer akitoa maelezo mafupi ya
Mchakato rasmi wa kumsaka Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula.
Wanao onekana Mbele ni
Baadhi ya wenyeji ambao ndio watakuwa wenyeji wa washiriki wa mama
shujaa wa chakula pindi watakapokuwa kijijini.
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam
Tanzania Jane Foster akiwashukuru wadau mbalimbali ambao wamefanikisha
mchakato mzima wa kuendesha shindano la Mama Shujaa wa Chakula, pia
kipekee amewashukuru wafanyakazi wa Oxfam akiwepo Eluka Kibona na
Suhaila Thawer kwa kuwa mstari wa mbele kufanikisha shindano hili na
mwisho kuwatakia kila la heri washiriki wote wanaokwenda katika
kushindana kumpata Mama Shujaa wa Chakula.
Washiriki wa Shindano la
Mama shujaa wakiwa wanatambulishwa tayari kuelekea Kisarawe Kijiji cha
Kisanga kwa ajili ya kumsaka mshindi ambapo Programu mzima itaoneshwa
katika Luninga ya ITV kila Siku kuanzia Tarehe 2.08.2015-21.08.2015
kuanzia saa 12 Jioni
Picha Na MoBlog
Post a Comment