HILI NDILO BALAA LA MAGUFULI KATIKA KAMPENI ZAKE MKOANI MBEYA

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akizungumza jambo na mlemavu wa miguu ndugu Joseph,mkazi wa kijiji cha Lwasho wilaya ya Momba,ambapo alimuahidi kumletea baiskeli ya kutembelea.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akiombewa na Watawa wa kijiji cha Lwasho,mara baada ya kumaliza mkutano wa kampeni katika kijiji cha Lwasho,wilaya ya Momba.

Palikuwa hapatoshi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchana wakati mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipowasili katika viwanja hivyo na kuwahutubia wananchi.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tunduma waliofurika kwa wingi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma,mkoa wa Mbeya mapema leo mchana,kwenye mkutano wa kampeni wa kuwaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano,ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Oktoba 25  mwaka huu.
Palikuwa hapatoshi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchana wakati mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipowasili katika viwanja hivyo na kuwahutubia wananchi.
 Maelfu ya Wananchi wa Tunduma waliojitokeza  kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika uwanja wa shule ya msingin Tunduma mkoani Mbeya.

   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya,Mh.Abbas Kandolo alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Nzoka Wilaya ya Momba mkoani humo,pichani kati ni Mgombea Ubunge wa jimbo la Mbozi Mh Godfrey Zambi.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Ileje Mh.Janet Mbene,mara baada ya kuwasili wilayani humo kuhutubia mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa wamefurika katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchama kumsikiliza mgombea urais wa CCM akimwaga sera zake kuwaomba Watanzania wamchague na kumpa ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano.
Wananchi wa wilaya ya Ileje wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa katumba,Ileje mjini wakimshangilia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni wilayani humo.

Post a Comment

Previous Post Next Post