Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John
Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Ludewa mjini kabla ya kuanza
kuwahutubia ,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo
na kuhudhriwa na maelfu ya watu.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John
Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Ludewa waliojitokeza kwa wingi
kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo.
Mgombea
Ubunge wa jimbo la Ludewa,aliyepita bila kupingwa Mh Deo Filikunjombe
,akisoma ilani ya CCM aliyokabidhiwa na Mgombea Urais wa CCM Dkt
Magufuli,wakati alipokuwa akihutubia wananchi wa kijiji cha Mlangali
wilayani Ludewa
Wananchi
wa mji wa Ludewa wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa mpira mjini
Ludewa wakimshangilia mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Msafara
wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukiwa umezuiwa na
Wananchi wa kijiji cha Mavanga wilayani Ludewa huku wakishangilia na
kuimba "JEMBE LA KAZI LIMEINGIA",ambapo Magufuli akiwa ameambatana na
Mbunge wa jimbo hilo la Ludewa,Mh Deo Filikunjombe walisimama na
kuzungumza na wananchi hao ikiwemo pia kuwaomba kura za kutosha ili
wapate ridhaa ya kuwaongoza Watanzania katika awamu ya tano.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya walemavu
waliokuwa wamefika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni kumsikiliza
sera zake,Dkt Magufulia alieleza kuwa katika Ilani ya CCM,kwa awamu ya
tano itawajali walemavu na kuwapa vipau mbele hasa katika masuala ya
elimu,ya kijamii pamoja na kuwawezesha kiuchumi ili waweze kujishulisha
vyema katika maisha yao ya kila siku
Wananchi
wa jimbo jipya la Madaba wakimsikiliza kwa makini mgombea Urais wa CCM
Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jukwaani kwenye mkutano
wa hadhara wa kampeni.
Wananchi
wa Mlangali wilayani Ludewa wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye
mkutano wa hdahara wa kampeni,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe
Magufuli aliwahutubia.
Mmoja
wa wakazi wa mji wa Ludewa akiwa na bendera yake,huku akimisikiliza
mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba ridhaa ya
kuwaongoza katika awamu ya tano kwa nafasi ya Urais.
Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukiwasili wilayani Ludewa kutoka mkoani Njombe.
Ngoma ya asili kutoka Ludewa ilipokuwa ikitumbuiza uwanjani hapo
Wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa hadhara wa kampeni.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John
Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Ludewa mjini kabla ya kuanza
kuwahutubia ,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo
na kuhudhriwa na maelfu ya watu.
Picha Na Michuzi
إرسال تعليق